Monday, December 28, 2015

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI IKULU LEO

2
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mh. Profesa Makame Mbarawa Ikulu, ambapo amewapisha mawaziri watano kujaza nafasi za mawaziri zilizokuwa wazi katika wizara kadhaa za serikali ya awamu ya tano, Hafla ya kuwaapisha mawaziri hao imefanyika leo asubuhi.

3
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mh. Gerson Lwenge kuongoza wizara hiyo ikulu leo asubuhi.
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango kuongoza wizara ya fedha.
5
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Dk. Joyce Nderichako.
6
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Naibu Waziri wa Wizara ya Ndani Hamad Yussuf Masauni.
7
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mawaziri walioapishwa katika picha wa pili kutoka kushoto ni Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan, wa pili kutoka kulia ni Mh. Majaliwa, Kassim Majaliwa Waziri Mkuu, Kulia ni Mh. Goerge Masaju Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mh. Ombeni Sefue.
8
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mawaziri walioapishwa pamoja na manaibu Waziri katika  wa pili kutoka kushoto ni Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan, wa pili kutoka kulia ni Mh. Majaliwa, Kassim Majaliwa Waziri Mkuu, Kulia ni Mh. Goerge Masaju Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mh. Ombeni Sefue.
9
Baadhi ya Mawaziri wakiwa wamekaa katika hafla hiyo kutoka kushoto ni Mh. Dk. Agustino Mahiga waziri wa mambo ya nje , Ushirikiano wa Kimataifa , Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kimataifa na Kikanda,  Mh. Dk. Harrison Mwakyembe Waziri wa Sheria na Katiba, Mh. Charles Kitwanga Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Injinia Edwin Mgonyani.
10
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mh. Waziri Mkuu Majaliwa, Kassim Majaliwa na Mwanasheria Mkuu wa serikali Mh. George Masaju katika hafla hiyo.
11
Mawaziri walioteuliwa wakisubiri kuapishwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli Ikulu leo jijini Dar es salaam. 
12
Baadhi ya waandishi wa habari waksubiri kushuhudia tukio hilo.
13
Mwanahabari Kissa Mwaipyana kutoka Chanel Ten alikuwa ni mmoja wa waandishi waliohudhuria hafla hiyo ya kuwaapisha mawaziri leo Ikulu.
14
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mh. Waziri Mkuu Majaliwa, Kassim Majaliwa
15
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiungumza na Mh. Dk. Agustino Mahiga waziri wa mambo ya nje , Ushirikiano wa Kimataifa , Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kimataifa na Kikanda
16
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiungumza na Mh. Dk. Harrison Mwakyembe Waziri wa Sheria na Katiba, kulia ni Mh. Dk. Agustino Mahiga waziri wa mambo ya nje , Ushirikiano wa Kimataifa , Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kimataifa na Kikanda
17
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisindikizwa na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa, Kassim Majaliwa kushoto na Mh. Dk. Agustino Mahiga waziri wa mambo ya nje , Ushirikiano wa Kimataifa , Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kimataifa na Kikanda wakati akiondoka ukumbini hapo mara baada ya kumaliza kazi ya kuwaapisha mawaziri.
18
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan  na Mh. Waziri Mkuu Majaliwa, Kassim Majaliwa alipokuwa akiondoka ukumbini mara baada ya kuwaapisha mawaziri.
19
Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango akihijiwa na waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa Ikulu leo.
20
Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Dk. Joyce Nderichako akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa ikulu leo.


No comments: