Monday, December 28, 2015

TIGO YAFIKIA WAFUASI MILIONI MOJA KATIKA MTANDAO WA FACEBOOK



Kampuni ya Tigo Tanzania hivi karibuni imetanga za kufikisha wafuasi milioni moja katika mtandao wao wa Facebook. Katika ukarasa wake wa Facebook, www.facebook.com/TigoTanzania kampuni ilifikisha mfuasi wa milioni  moja Jumapili Desemba 27 mwaka huu hapa Tanzania.

Kutokana na ongezeko la matumizi ya mtandao wa kijamii wa Facebook hapan chini, Facebook imekuwa mstari wa mbele  katika matumizi kutoka na uzinduzi wa Facebook katika lugha ya Kiswahili uliofanyika mwaka wa 2014 kwa ushirikiano wa Tigo Tanzania na Facebook, ambapo wateja wanaweza kutumia Facebook kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza kupitia simu zao za mkononi bila malipo yoyote ya ziada.

 Ukurasa wa Facebook wa Tigo uliundwa Juni 2011 na umekuwa jukwaa madhubuti wa kurambaza na wateja wake wapendwa ambapo wanajifunza kuhusu huduma na bidhaa mpya za kampuni.

Hivi karibuni, Tigo Tanzania imejishindia tuzo mbili katika Tuzo za Uongozi Bora (Tanzania Leadership Awards) ambayo inatambua mashirika na watu binafsi katika uongozi. Tuzo hizo ni ya Ubora wa bidhaa (The Hall of Fame in Brand Excellence), na Matumizi Bora ya Mitandao ya Kijamii Katika Mauzo( Best use of Social Media in Marketing).

Tigo Tanzania inaongoza katika soko la mawasiliano na imekuwa mstari wambele katika mitandao ya kijamii ambapo wateja wamekuwa wakiuliza maswali na kujibiwa haraka. Hii imeufanya mtandao kuaminika sana na wateja na kutumika kama mwendelezo wa huduma kwa wateja.
Kuhusu Facebook Mkurugenzi wa Tigo Bwana Diego Gutierrez anasema. “Jukwaa letu la Facebook na Twitter (Tigo TZ) limekuwa kitendea kazi muhimu ambacho kinatumika kujifunza kutoka  kwa wateja wetu na jamii kwa jumla ambao wanakitumia.
Tunajivunia kwa kuweza kuyafikia mafanikio haya, na tunawashukuru wateja wetu kwa kuwa naimani nasi.

Tigo, imedhamiria kubadilisha mtindo wa maisha wakidijitali kwa kuwa letea wateja wetu ubunifu wa teknolojia maridha wa. Hivi karibuni, tumezindua teknolojia ya 4G LTE hapa Tanzania ambayo ni intaneti iliyona kasi kuliko zote pamoja na ofa ya aina ya simu yaTechno Y3 Smartphone inayotumia lugha ya Kiswahili.

No comments: