Saturday, December 19, 2015

UKAWA wapeleka Mafuriko Masasi Jioni hii,Tizama Funga Kampeni ya uchaguzi mdogo wa masasi leo

Selemani Bungala (Bwege) wa Kilwa Kusini kupitia Chama cha Wananchi (CUF) akihutubia maelfu na wakazi wa masasi jioni ya leo

Idadi kubwa ya wakazi wa jimbo la Masasi na Viunga vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika uwanja wa mti wa mwiba jimboni hapo katika mkutano  wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge ndani ya Jimbo hilo la Masasi

Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mh HAMIDU BOBANI akiwahutubia wakazi maelfu waliojitokeza katika mkutano huo ambao ulihudhuriwa pia na Wabunge wote wa upinzani kutoka Lindi,na mtwara Pamoja na wabunge wa zanzibar pamoja na mbunge wa kindondoni Jijini Dar es salaam

Mbunge wa jimbo la Kinondoni Jijini Dar es salaam kutoka chama cha wananchi CUF ndani ya umoja wa vyama vya UKAWA Mh MAULID MTULIA akiwahutubia maefu wa wafuasi wa vyama hivyo katika mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge ndani ya jimbo la Masasi ambapo uchaguzi huo unafanyika kutokana na aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo EMANUEL MAKAIDI kufariki dunia wakati wa uchaguzi mkuu uliomalizika mwaka huu.


Mbunge wa Jimbo la ndanda Mh CECIL MWAMBE akiwahutubia maelfu ya wafuasi wa vyama vya Ukawa katika mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo katika jimbo la masasi,Mkutano uliofanyika katika uwanja wa mti wa mwiba Jimboni humo
Polisi wakiranda randa wakati wa mkutano huo uliokuwa wa kufunga kampeni katika jimbo la masasi



No comments: