Sunday, December 20, 2015

Urembo--Mwanamitindo TAUSI LIKOKOLA sasa amekuja na Aina hii ya nywele kwa ajili ya wanawake wa kitanzania,zimezinduliwa Rasmi,Tukio nzima liko hapa

 Mwananitindo mkongwe na mkubwa nchini Tanzania ambaye amekuwa akifanya shughuli zake nje ya Tanzania kwa muda mrefu TAUSI LIKOKOLA kupitia kampuni yake ya TAUSI DREAMS hatimaye amezindua aina mpya ya nywele kwa ajili ya wanawake nchini uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa wiki hii jijini Dar es salaam ambapo ni muendelezo wa mwanamitindo huyo kuendelea kuwekeza katika urembo nchini.

Uzinduzi huo ulifanyika katika duka linakopatikana aina ya nywele hizo ambazo amezipa jina la TAUSI BEAUTFULL YOU HAIR lililopo ndani ya Osterbay shoping center Jijini Dar es salaam na kuhudhiriwa na wadau mbalimbali wa maswala ya urembo nchini.

Akizungumza na mtandao huu wakati akitambulisha ujio mpya wa nywele hizo Mrembo huyo amesema kuwa kabla ya kufanya uamuzi wa kuwekeza katika nywele alianza kwa kufanya utafiti nchini marekani na duniani ili kujua aina ipi ya nywele inayoweza kumfaa mwanamke wa kiafrica na hususani Tanzania ambapo alizunguka nchini marekani na kuona jinsi nywele zinavyoandaliwa kwa ajili ya kuuzwa na hatimaye akafanikiwa kupata aina hiyo ya nywele ambayo amesema ni nywele asili ya binadamu tofauti na aina nyingine ambazo zimekuwa ni nywele bandia.


Akitaja bei za aina hiyo ya nywele amesema kuwa zitakuwa zikianzia dola 150 ambazo ni sawa na laki tatu za kitanzania kwa Bandle moja ambapo amesema kuwa bado bei hiyo ni nafuu kulingana na bei za aina nyingine za nywele nchini pamoja na ubora wa nywele zake ambapo amesema kuwa amelenga sana wadada wanaojipenda na kujali urembo wao wa nywele.

Aidha amesema kuwa aina hiyo ya nywele ni bora na imara ukilinganisha na aina nyingi ya nywele iliyopo nchini kwa sasa hivyo akawataka wanawake wa kitanzania kuhakikiaha kuwa wanachagua kilicho bora kwa urembo wao wa kila siku.
ENDELEA KUTIZAMA PICHA ZA UZINDUZI.Enjoy
































No comments: