Sunday, January 17, 2016

Habari kubwa muda huu--Gazeti La Mawio lafutwa Rasmi Tanzania,Wahariri wake wasakwa usiku na mchana na Polisi.

WAZIRI wa Habari,utamaduni,sanaa na michezo,Nape Nnauye akizngumza na wanahabari Mapema Leo Jijini Dar es salaam kuhusu kulifuta Gazeti La mawio katika Orodha ya magazeti nchini Tanzania
NA KAROLI VINSENT
WAZIRI wa Habari,utamaduni,sanaa na michezo,Nape Nnauye ametaja sababu ya serikali kulifuta  Gazeti la Mawio kwenye orodha ya msajili wa magazeti  nchini kwa kusema wahariri wa Gazeti hilo wa wamekuwa na kiburi kwa serikali wanapotakiwa kujitetea kuhusu habari wanazoandika.

Akizungumza na waandishi wa habari mda huu jijini Dar es Salaam,waziri Nnauye amesema serikali imefikia hatua ya kulifuta gazeti hilo kwenye orodha ya msajili wa magazeti pamoja na kulizuia kutochapishwa kwenye mitandao.

“Sheria ya magazeti ya mwaka 1976 sura ya 229 kifungu cha 25 (i) kinamenipa mamlaka ya kulifungia gazeti hili,kwahiyo  kwaanzia tarehe 15 January mwaka huu tumelifuta  kwenye orodha ya magazeti ya msajili,kwahiyo tumelipiga marufuku hata kuchapisha kwenye mtandao’amesema Waziri.

Waziri Nnauye ameyataja makosa yaliyopelekea serikali mpaka kuchukua hatua hiyo,ni baada ya ofisi ya msajili wa magazeti kuwaandikia barua wahariri wa gazeti hilo kwa kuwataka kusahihisha makosa yao tangu mwaka 2013 jambo analodai kuwa wahariri wake walikuwa wanaijibu majibu mabaya serikali.

“Yaani wahariri wa hili gazeti tangu mwaka 2013 tunawaambia wabadilishe aina ya uandishi wa habari lakini wakawa wanaijibu serikali majibu mabaya na wakawa wanaendelea kuandika habari ya uchochezi na kuharibu amani ya nchi,”
Hata hivyo,Waziri Nnauye amevitaka vyombo vya habari pamoja na wahariri kuzingatia sheria na kanuni za taratibu za nchi kwa kuandika habari zenye kufuata weledi.


     WAHARIRI WA MAWIO WANATAFUTWA.

Taarifa ambazo Fullhabari.blog  imezipata zinasema Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawatafuta wahariri wa gazeti la mawio ambao ni Saimon Mkina na Jabir Idrissa kwa kosa la  kuandika kwenye gazeti hilo toleo 152 ya  Alhamisi ya tarehe 13 mwezi junuary mwaka huu yenye 
kichwa cha habari MACHAFUKO YAJA ZANZIBAR.
‘Ninachokwambia tangu juzi ijumaa wamekuja polisi wamevamia kwenye ofisi zetu mbili za magomeni na ile ya pale mwananyamala wanakuja kuwasaka hawa wahariri wetu na wamewakosa”amesema mtoa taarifa wetu wa Gazeti la Mawio.

    MMILIKI WA MAWIO WANENA.

Akizungumza na Fullhabari.blogs kwa sharti la kutotaja jina lake Mtandaoni mmliki mmoja wapo wa Gazeti hilo,amesema kwa sasa wanajipanga kulifufua gazeti moja wapo ambalo litaaendelea na kazi zilizokuwa zikifanywa na gazeti lililofungiwa .

“Tumepokea kwa masikitiko makubwa kwa kufungiwa gazeti letu,ila tupo mbioni kufufua gazeti moja wapo lilokufa,na kuhakikishia alhamisi tunaendelea tena utashangaa ndugu”
Aidha akijibu kuhusu swalila mwandishi wa habarti alilotaka kujua kamawanaruhusiwa kufungua gazeti linguine na kuendelea na kazi waziri NAPE amesema kuwa sheria inaruhusu mtu kufungua gazeti na hawana kipingamizi japo hakuweka wazi hatua ambazo watachukua kama wakifungua na kuendelea kufanya hivyo.

No comments: