Saturday, February 20, 2016

ACT YAMSIMAMISHA UANACHAMA MGOMBEA URAIS ZANZIBAR


Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT - Wazalendo) katika kikao chake cha Kamati Maalum ya Zanzibar cha tarehe 19 Februari, 2016 kimepokea taarifa rasmi kuwa aliyekuwa mgombea wa urais wa zanzibar ndugu Khamis Idd Lila kwa kushirikiana na ndugu Ali makame Issa huku wakitambua msimamo wa Chama kwa makusudi wameamua kupingana na msimamo huo kwa maslahi yao binafsi na kukidhalilisha na kuingiza mgogoro usiokuwa na sababu kwa kuandika barua ya kushiriki uchaguzi wa marudio ambao Chama kilishapeleka barua rasmi tarehe 09 Februari,2016 ya kutoshiriki uchaguzi huo.



Kwa kitendo chao hicho na kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na maadili ya chama Kamati maalum ya Zanzibar imewasimamisha rasmi uanachama kwa mujibu wa katiba ya ACT Ibara ya 11 (2) kuanzia leo tarehe 19 Februri,2016 kwa ukiukwaji mkubwa wa katiba Ibara ya 7(3)(5)(9),ibara ya 10 (2)(c)(d),Ibara ya 22(1)(2)(4).

Kwa mujibu wa Katiba ya ACT Wazalendo masuala yote ya kinadhamu kwa viongozi na wanachama yanashughulikiwa na Kamati za uadilifu za ngazi husika na kwa kuwa kwa sasa Kamati hizo hazijaundwa Kamati ya Uongozi ya Taifa ndio inayoshughulikia na mambo yote ya kinidhamu.

Hivyo jambo hili linawasilishwa mbele ya Kamati ya Uongozi ya Taifa kwa hatua zaidi na kwa taarifa zaidi naambatanisha na tamko la Chama katika kikao cha tarehe 13 Februari,2016 kilichofanyika Dar es Salaam.
Imetolewa leo tarehe 20 Februari, 2016
Juma Said Sanani
Naibu Katibu Mkuu 
Zanzibar

No comments: