Jumuiya ya wanawake wa
chama cha wananchi CUF maarufu kama JUKECUF wametangaza kufanya maandamano ya Amani
siku ya tarehe 22,mwezi huu wa pili Jijini Dar es salaam yenye adhma ya kupinga
hali ya kisiasa inayoendelea visiwani Zanzibar.
Akizungumza na wanahabari
mapema leo mwenyekiti wa jumuiya hiyo Mh
severena mwijage amewaambia wanahabari kuwa maandamano hayo yataanzia ofisi kuu
za CUF buguruni kuelekea ofisi ya makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
Mh SAMIA SULUHU
Amesema kuwa jumuiya hiyo
inatambua kwamba hali ya Amani iliyopo Zanzibar ikivurugika kwa kiasi kikubwa watakaoathirika
ni kina mama na watoto hivyo wameona ni
bora kufikisha kilo chao hicho kwa makamu wa Rais ambaye ni Mwanamke mwenzao
awasaidie.
Maandamano hayo yatapita
barabara ya uhuru,ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es salaam,karume,kariakoo,mnazi
mmoja,Central polisi,barabara ya sokoine ,Bandarini,mahakama kuu,mahakama ya
ardhi,Hadi ofisi ya makamu wa Rais.
Maandamano hayo bado
hayajaruhusiwa na polisi licha ya polisi kupata marua kutoka CUF.
No comments:
Post a Comment