Thursday, February 18, 2016

Tigo yatahadharisha wateja dhidi ya matumizi ya simu bandia


Mkuu wa  Kitengo cha Vifaa vya Mawasiliano wa TigoDavid Zakaria akielezea athari  za matumizi ya  simu bandia kwa waandishi wa habari  (Hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika mapema leo katika makao makuu ya Tigo Kijitonyama Dar es salaam., kushoto kwake ni Meneja wa Mawasiliano, John Wanyancha
 
…………………………………………………………………………………………………………..
Watumiaji wa simu za mkononi wameonywa dhidi
ya matumizi ya simu bandia na zisisokidhi viwango vya ubora ambazo tayari
zimetangwa kupigwa marufuku na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuanzia
mwezi Juni mwaka huu.
Kutokana na sababu hiyo, Tigo, ambayo ni kampuni ya kidijitali,
imeanza kuendesha kampeni ya kuhamasisisha wateja wake na umma kwa jumla kupitia
vyombo vya Habari inayolenga kuwaepusha na athari za matumizi ya simu bandia.
 
 “Kwa mujibu wa maelekezo ya
TCRA matumizi ya simu za mkononi ambazo namba zake za utambulisho wa kimataifa
(IMEI) ni bandia yatapigwa marufuku kutumika kwa mitandao yote ya simu nchini
Tanzania kuanzia Juni 16 mwaka huu. Ili kujiepusha na usumbufu wowote
utakaotokana na hatua hii tunawashauri wateja wetu kujipatia simu halisi na
bora kutoka maduka ya Tigo yaliyo karibu nao,“ alisema Mkuu wa  Kitengo cha Vifaa vya Mawasiliano wa Tigo, David Zakaria.
Ripoti ya utafiti ulichapishwa katika tovuti ya GSMA (“http://www.gsma.comwww.gsma.com ) inasema kwamba tofauti na ilivyo
kwa simu halali ambazo hupitia mamia ya hatua mbalimbali za kuhakiki ubora wake
kabla ya kupelekwa sokoni, simu bandia hazifanyiwi majarbio ya ubora na kuna taarifa
za kitafiti zinazoonyesha kuwa baadhi ya simu bandia zina kiwango kikubwa cha
madini ya risasi na vitu vingine ambavyo ni hatari kwa mazingira na afya ya
binadamu.
Ripoti hiyo inaendelea kusema kuwa simu feki zinatengenezwa na
malighafi dhaifu zisizokidhi viwango na zimeshaonesha kuwa kiwango cha hatari
cha vyuma na kemikali kama risasi hadi kufikia kiwango cha mara 40 zaidi kuliko
kiwango kilichoidhinishwa na sekta ya mawasiliano duniani kwa mujibu wa na
Jukwaa la Watengenezaji wa Simu za Mkononi (MMF).
Akizungumza kuhusu hatua ya Tigo kutoa tahadhari kwa wateja wake
Zakaria alisema, “Wanunuzi wanatakiwa kuwa waangalifu wakati wanaponunua simu
mpya au vifaa vya mawasiliano madukani au katika intaneti kwa sababu bidhaa
nyingi feki zinatengenezwa kwa kuigaa muundo na nembo za kibiashara za bidhaa
halisi kwa makusudi ili kuwalaghai wateja.
“Ili kuweza kuelewa iwapo simu yako ni feki au ni halisi unatakiwa
kupiga namba namba *#06# ambapo atapokea
namba ya IMEI ya simu hiyo na kisha kutima kwa njia ya jumbe mfupi
kwenda namba 15090 ambapo utapata jibu iwapo simu hiyo ya mkononi ni halisi au
ni bandia,” alisema Zacharia.

No comments: