NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. ASHANTU KIJAJI AFUNGUA MKUTANO WA 25 WA MWAKA WA WADAU NA WANACHAMA WAMFUKO WA PENSHENI WA PPF,JIJINI DAR.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu wa 25 wa mwaka wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ulioanza jijini Dar es Salaam, leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,  unaomalizika kesho. 

Picha ya pamoja na wadau baada ya ufunguzi wa mkutano huo. 

Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wadau waliopata Vyeti katika ufunguzi huo. 

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashantu Kijaji (wa pili kulia) akimkabidhi Cheti za mshindi wa pili wa Usafirishaji,Mawasiliano na Uzalishaji Umeme, Ofisa wa kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel, Pamela Mwandetele, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 25 wa mwaka wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ulioanza jijini Dar es Salaam, leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,  unaomalizika kesho. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio. 

Baadhi ya Wadau na Wanachama wa Mfuko huowakimsikiliza Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi huo leo kwenye Ukumbi wa  Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere. 

 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashantu Kijaji (wa pili kulia) akimkabidhi Cheti za mshindi wa kwanza wajumla Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu Charles Kazuka, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 25 wa mwaka wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ulioanza jijini Dar es Salaam, leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,  unaomalizika kesho. Wa pili (kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (wa pili kushoto) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhani Kijjah. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Richard Ndasa. 

Mwanachama wa PPF, Bakari Kaoneka, akitoa ushuhuda wa Fao la Uzeeni , wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. 

 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashantu Kijaji (Mb) akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa 25 wa mwaka wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ulioanza jijini Dar es Salaam, leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,  unaomalizika kesho. Akizungumza wakati wa mkutano huo Dkt.Kijaji aliupongeza Mfuko huo wa PPF kwa mikakati thabiti ya kutoa huduma zake kwaJamii. 

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu wa 25 wa mwaka wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ulioanza jijini Dar es Salaam, leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,  unaomalizika kesho. 


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashantu Kijaji (wa pili kulia) akimkabidhi Cheti za mshindi wa kwanza wajumla Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu Charles Kazuka, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 25 wa mwaka wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ulioanza jijini Dar es Salaam, leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,  unaomalizika kesho. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (wa pili kushoto) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhani Kijjah. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhani Kijjah, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu wa 25 wa mwaka wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ulioanza jijini Dar es Salaam, leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,  unaomalizika kesho. 


Mwanachama wa PPF, Angela Mgulu, akitoa ushuhuda wa Fao la Uzazi , wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. 
HOTUBA
YA
MGENI RASMI
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO
MHESHIMIWA DKT. ASHATU KIJAJI (Mb)
WAKATI WA UFUNGUZI
WA
MKUTANO WA 25
WA MWAKA WA WANACHAMA NA WADAU WA
MFUKO WA PENSHENI WA PPFMwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ndugu Ramadhani Khijjah;
Ndugu Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF;
Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) ;
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi Irene Isaka;
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ndugu William Erio;
Viongozi wote wa Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Vyama vya Wafanyakazi mliopo hapa;
Ndugu Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF;
Watoa Mada na Wajadili Mada;
Washiriki wa Mkutano huu;
Wanahabari;
Wafanyakazi wa PPF;
Mabibi na Mabwana.


Awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kukushukuru wewe binafsi Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Wajumbe wa Bodi yako na Menejimenti ya Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa heshima mliyonipa ya kunialika kuja kufungua mkutano wenu huu wa 25 wa mwaka wa Wanachama na Wadau wa PPF. 

Nichukue pia fursa hii kwa niaba ya Serikali ya awamu ya tano kuwashukuru wanachama na wadau wote kwa kufika na kushiriki kwenye mkutano huu wa 25 wa mwaka wa wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF.

Aidha ningependa kuupongeza Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa kuandaa mkutano huu wa kila mwaka kwa mara ya 25 mfulululizo.  Sote tunafahamu kuwa, mikutano ya namna hii ni muhimu kwa ajili ya ushirikishwaji, ubadilishanaji mawazo na kupokea maoni kwa nia ya kuboresha utendaji na utoaji huduma kwa wananchama na jamii kwa ujumla.   Utaratibu huu unaimarisha uwazi na uwajibikaji na kuongeza imani ya wananchi na wanachama kwa Mifuko yao.

Ndugu Mwenyekiti wa Bodi, wakati unanikaribisha pamoja na mambo mengine umeelezea ushiriki wa PPF katika kutekeleza mada kuu na kwa kifupi umeweza kuelezea mafanikio ambayo Mfuko umeyapata tangu Mkutano uliopita. Umeeleza jinsi Mfuko wenu ulivyoweza kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu hii ili kuendana na mabadiliko yanayotokea kwenye jamii pamoja na mafanikio ya Mfuko wa Pensheni wa PPF tangu mkutano uliopita ambayo ni kuongezeka kwa mapato yanayotokana na michango na uwekezaji, kukua kwa thamani ya Mfuko wa PPF na kufikia zaidi ya shilingi trillioni mbili hadi mwishoni mwa Juni 2015. Nawapongeza sana kwa mafanikio hayo hususani kwenye uwekezaji wenye tija eneo ambalo lina matatizo kwenye Taasisi nyingi.

Vilevile umeelezea jinsi Mfuko wenu ulivyojikita katika matumizi ya TEHAMA kwenye utoaji wa huduma; kutanua wigo wa kuwasomesha watoto wa wanachama wenu wanaofariki wakiwa kwenye ajira; kuendelea kutoa mikopo ya SACCOS ambapo mpaka sasa mmetoa jumla ya shilingi bilioni 91.34 kwa wanachama wenu, kuanzishwa kwa mfumo mpya wa “Wote Scheme “ kwa sekta isiyokuwa rasmi, na mafao mapya ya Uzazi. Huu ni ubunifu wa hali ya juu unavyoonesha jinsi mnavyowajali wanachama wenu.Kwa niaba ya Serikali napenda kuwapongeza sana kwa mafanikio hayo.

Mambo hayo niliyoyataja pamoja na Taarifa yako kuwa Mfuko wenu umeshapata tuzo tatu za kimataifa kutoka Shirikisho la Hifadhi ya Jamii duniani (ISSA) na tuzo mbili za hesabu bora kwa  miaka miwili mfululizo kutoka Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa ndani (NBAA), na kuwa sasa huduma zenu ni za kiwango cha kimataifa kama inavyodhihirishwa na cheti utoaji huduma bora cha kimataifa ( ISO 9001: 2008 Certified) yamenifurahisha sana.

Kwa niaba ya Wizara ya Fedha napenda kuwaarifu kuwa Serikali ina  imani na utendaji mzuri wa Mfuko wenu na naipongeza sana Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa PPF kwa hilo

Ni wazi kuwa wadau mlioko hapa na wengine watakaopata Taarifa hizi kupitia kwenye vyombo vya habari watachangamkia fursa ya kujiunga na Mfuko wa PPF ili  waweze kunufaika na huduma za kisasa na mafao bora yanayotolewa na Mfuko wenu. 

Ndugu Mwenyekiti wa Bodi, nimalizie kwa kuzungumzia baadhi ya changamoto ulizozitaja kama ifuatavyo:
(i)          Kuhusu waaajiri wasioleta michango kwa wakati ninaagiza kwamba waajiri wa namna hiyo waache tabia hiyo mara moja kwani ni uvunjaji wa sheria na unaleta usumbufu usio wa lazima kwa wastaafu na Mifuko. Serikali imeshatoa agizo la kuwataka waajiri wote kuhahakisha wana mikataba na wafanyakazi wao na wanawaandikisha katika Mifuko ya hifadhi ya jamii na kuwachangia kama sheria inavyotaka. Ninaagiza kwamba hatua za kisheria zichukuliwe kwa kuwashtaki waajiri wote wanaochelewesha michango na kuziomba mahakama kesi hizo ziamuliwe kwa haraka ili kuondoa kero kwa wananchi na Mifuko.Waajiri wakichangia kwa mujibu wa sheria watawawezesha wanachama kupata mafao yao kikamilifu na kwa wakati; wakati huo huo kuifanya mifuko kubuni mafao zaidi kwa wanachama badala ya kutumia muda mrefu kufuatilia kesi za michango mahakamani.

(ii)         Kuhusu madeni ya  Serikali kwa PPF,tayari suala hili linashughulikiwa ambapo tayari Wizara imeshaiagiza Benki Kuu kuandaa non-cash bond  ambayo itatolewa kwa Mfuko ikiwa ni mkakati wa kulipa madeni hayo.Pia Serikali imeshaanza na itaendelea kuhakikisha michango ya pensheni kwa wafanyakazi wa taasisi zinazopata ruzuku kutoka Serikalini inalipwa kwa wakati.

(iii)        Kuhusu suala la mafao ya kujitoa, Wizara yangu itawasiliana na  Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu ili kupata ufumbuzi wa kudumu wa suala hili kwani ni dhahiri kuwa linakwenda kinyume cha kanuni za hifadhi ya jamii duniani na halina tija kwa wafanyakazi na Mifuko.

Naomba kabla sijamaliza nami niwape changamoto zifuatazo:

i)             Mfuko uendelee kuboresha huduma kwa wanachama wake kwa kuzingatia mahitaji ya sasa ili kuwavuta watu wengi zaidi kujiunga na PPF

ii)           Kwa kuzingatia mada kuu ya mkutano, Mfuko uangalie uwekezaji katika maeneo ambayo bado haujaingia kwa kuzingatia kanuni za uwekezaji zilizotolewa na Benki Kuu ya Tanzania kwa kushirikiana na SSRA baada ya kujidhihirisha kuwa uwekezaji huo utakuwa na tija ili kujiongezea mapato na hivyo kuwa na uwezo mzuri zaidi wa kuboresha mafao kwa wanachama wake.

Baada ya kusema maneno hayo, naomba sasa kutamka kwamba mkutano huu wa 25 wa mwaka wa wanachama na wadau wa PPF umefunguliwa rasmi.
Asanteni sana kwa kunisikiliza.    

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.