Friday, February 26, 2016

SDL KUMALIZIKA WIKIENDI HII


Ligi Daraja la Pili (SDL) inatarajiwa kumalizika wikiendi hii kwa michezo 12 kuchezwa katika makundi ya A, B, C & D katika viwanja mbalimbali nchini, huku kila kundi likitoa timu moja ya juu itakayocheza fainali za kupanda ligi daraja la kwanza msimu ujao.

Kesho Ijumaa, michezo mitatu ya kundi C itachezwa katika raundi hiyo ya mwisho, Villa Squad watacheza dhidi ya Mshikamano (Mabatini, Mlandizi), Abajalo Dar v Karikaoo FC (Karume) na Changanyikeni watakuwa wenyeji wa Cosmopolitan katika uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha.
Kundi A, Jumamosi Green Warriors watawakaribisha Abajaro Tabora katika uwanja wa Mabatini Mlandizi, Transit Camp watakua wenyeji wa Mvuvumwa uwanja wa Kambarage Shinyanga, huku siku ya Alhamis Singida United watacheza dhidi ya Mirambo uwanja wa Namfua mjini Singida.
Jumamosi Kundi C, Alliance Schools watakua wneyeji wa Bulyankulu katika uwanja wa CCM Kirumba, JKT Rwamkoma watacheza dhidi ya  Pamba FC uwanja wa Karume Musoma, na Madini FC watakua wenyeji wa AFC Arusha uwanja wa Mbulu.
Kundi D, Jumapili Mkamba Rangers watacheza dhidi ya Wenda FC uwanja wa CCM Mkamba, Sabasaba watakua wenyeji wa The Mighty Elephant uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, huku Mbeya Warriors wakicheza dhidi ya African Wanderes katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Timu moja ya kwanza kutoka katika kila kundi zitacheza hatua ya Fainali Machi 7-14, 2015 uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, ili kupata timu tatu za juu zitakazopanda moja kwa moja ligi daraja la kwanza (StarTimes League) msimu ujao.

No comments: