Monday, March 7, 2016

KAIRUKI-KATIBA MPYA ITALETA USAWA WA KIJINSIA NCHINI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora MH ANGELA KAIRUKI akitoa mchango wake katika majadiliano hayo yaliyoandaliwa na mtandao wa TGNP kwa ajili ya kujadili maswala mbalimbali ya kijinsia kuelekea kuadhimisha siku ya wanawake duniani hapo kesho
Na Exaud Mtei (Msaka Habari)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora MH ANGELA KAIRUKI amesema kuwa lengo la kufikia 50 kwa 50 baina ya wanawake na wanaume litafikiwa ncini Tanzania endapo watanzania wataipitisha katiba pendekezwa iwe katiba mpya ya Tanzania kwani imejaa haki za usawa na kijinsia.

Waziri Kairuki ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam katika majadiliano yaliyoandaliwa na mtandao wa kijisia nchini TGNP kwa lengo la kujadili mambo mbalmbali yanayohusu usawa wa kijinsia ikiwa ni siku moja kabla ya dunia kuadhimisha siku ya wanawake duniani,majadiliano ambayo yaliwahusisha wadau mbalimbali wa maswala hayo
Ruth Meena Ni moja kati ya wanaharakati waliotoa mchango wao leo
Amesema kuwa kwa mujibu wa katiba pendekezwa imeweka wazi maswala ya usawa wa kijinsia hususani katika ngazi za uongozi ambapo katika swala la wabunge katiba hiyo imeeleza wazi kuwa kila jimbo litakuwa na wabunge wawili mwanawake na mwanaume jambo ambalo litasaidia kuweka haki na usawa wa kijinsia katika nchi.
Mwenyekiti wa bodi ya TGNP Mama MERRY RUSIMBI akizzungumza wakati wa mdalada huo uliofanyika makao makuu ya TGNP Jijini Dar es salaam
Ameongeza kuwa katika serikali ya awamu ya tano imeanza kuonyesha mfano kwa kuwajali wanawake kwa kuanza na kumpa mwanamke nafasi ya kuwa makamu wa Rais jambo ambalo limeanza kuoonyesha njia na kutia moyo kuelekea malengo ya 50 kwa 50 nchini.

Amesema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa wanamuwezesha mwanamke katika secta mbalimbali ikiwemo swala la kiuchumi na kujikwamua na umaskini,kuwawezesha katika elimu na kujitambu pamoja na kuwasaidia kuwaondoa katika maswala ya ukatili wa kijinsia.
GENERAL ULIMWENGU ambayo ni mpigania ukombozi nchini alikuwepo
Katika majadiliano hayo pia yalihudhruwa na wanaharakati mbalimbali wa maswala ya jinsia akiwemo GENERAL ULIMWENGU ambayo ni mpigania ukombozi nchini ambapo akizungumza katika mjadala huo amesema kuwa mila na tamaduni za Tanzania pamoja na kufanyishwa kazi sana wanawake kuliko wanaume imekuwa ni moja kati ya mambo yanayodidimiza na na kushusha jitihada za kumwezesha mwananke nchini Tanzania.
Siku ya wanawake Dunia inaadhimishwa kila ifikapo Tarehe 8 mwezi kila mwaka  wa tatu kote duniani huku kauli mbiu ya maadhimisho hayo nchini Tanzania 50/50 ifikapo 2030 tuongeze jitihada.


No comments: