MSTAHIKI meya wa halmashauri ya Temeke Abdalah Chaurembo amelitaka balaza la madiwani kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato katika kata zao


                                                                                                                     MSTAHIKI meya wa halmashauri ya Temeke Abdalah Chaurembo amelitaka balaza la madiwani kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato katika kata zao ili kuboresha na kukuza mapato yao ya ndani  kwaajili ya kuweza kufikia malengo yao ya kutekeleza shughuli za maendeleo ya jamii.

Hayo aliyasema jana  na mstahiki meya huyo wakati wa balaza la madiwani katika kujadili makadirio ya mapato na matumizi ya kawaida pamoja na miradi ya maendeleo kwa mwaka 2016/2017.

Akizungumza na madiwani wa balaza hilo Mstahiki meya wa Temeke,alisema kuwa madiwani wanatakiwa kufuatilia ukusanyaji wa mapato kwa kuwabana watendaji wao ili  kuongeza jitihada katika kuhakikisha halmashauri yake inapata fedha za kutosha za kuboresha shughuli mbali mbali za kijamii katika kipindi cha mwaka wa
fedha wa 2016/2017.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya  Manispaa ya Temeke Photidas Kagimbo alisema kuwa makadirio ya mapato ya  Halmashauri yake kwa mwaka 2016/2017 ni
sh bil 231,685,350,340.00 ambapo sh bil 50,285,639,000.00  ni sawa na asilimia 21 ni  mapato kutoka vyanzo vyandani,ruzuku kutoka serikali kuu na mishahara nibil 105,151,112,288.00,fedha za maendeleo ni bil 18,542,688,852,00,Bil 57,069,696,000.00 miradi ya DMDP,na wafadhili ni sh  mil 636,204,200.00.

Alisema kuwa Halmashauri yake imejipanga kuongeza nguvu katika kusimamia ukusanyaji wa kodi ikiwemo kuchukua hatua za kisheria kwa wafanyabiashara wanaokwepa kulipakodi kwakuwa shughuli za maendeleo ya nchi yanatokana na kodi hivyo ni muhimu kila jamii kutambua umuhimu wa kulipa kodi ili kuchochea kuongezeka kwa shughuli za maendeleo
ya taifa letu.
Naye Diwani wa kata ya mbagala kuu Yusuph Manji amemtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kutafuta namna na njia mbadala za kuhakikisha Manispaa ya Temeke inakuwa na mifumo mizuri itakayoiwezesha kujitegemea katika kusimamia shughuli za maendeleo ya ndani bila kuwa tegemezi kwa wafadhili na serikali kuu.

"kwa mujibu wa tamko la mkuu wa mkoa kwamba halmashauri zinatakiwa kujitegemea zenyewe ili kupunguza utegemezi kutoka serikali kuu,na wafadhili hivyo lazima kuboresha ukusanyaji wa mapato
ya ndani"alisema.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.