Tuesday, March 29, 2016

SERIKALI YA TANZANIA KUJENGA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA TANGA HADI UGANDA.

1Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa akiongea na baadhi waandishi wa habari  mara baada mkutano ya wafanyabiashara wa sekta ya mafuta nchini leo jijini Dar es salaam.
2Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Sekta ya Mafuta nchini Dkt. Gideon Kaunda akiongea na baadhi waandishi wa habari  mara baada mkutano ya wafanyabiashara wa sekta ya mafuta nchini leo jijini Dar es salaam.
Picha na Ally Daud- Maelezo

……………………………………………………………….
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
SERIKALI za Tanzania na Uganda zinatarajia kuanzisha mradi wa uwekezaji wa ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta unaolenga kuongeza pato la taifa na uchumi wa nchi hizo.
Mradi huo unatarajia kugharimu kiasi cha Dola za Marekani bilioni nne na utekelezaji wake utaanza mwanzoni mwa mwaka 2017.
Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu (Machi 28, 2016) Jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa alipokuwa na akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wake na wafanyabiashara wa sekta ya mafuta nchini.
Prof. Ntalikwa amezitaja fursa ambazo zitanufaisha taifa kuwa ni pamoja na kodi zitakazolipwa, kuongezeka kwa wigo wa ajira kupitia miradi huo pamoja na tenda mbalimbali zitakazotolewa wakati na baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo.
 “Tanzania ina kila sababu ya kupata mradi huo kwa kuwa ina uzoefu wa kuwa na mabomba kama hayo manne nchini na tunajivunia bandari yetu ya Tanga yenye kina kirefu kuliko bandari zote Afrika Mashariki” alisema Prof. Ntalikwa.
Prof. Ntalikwa amesema kuwa mwitikio wa wafanyabishara wa sekta ya mafuta nchini ni mzuri na kubainisha kuwa wanatarajia kusafiri kuelekea nchini Uganda kujionea fursa mbalimbali zinazopatikana nchini humo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa sekta ya mafuta nchini Dkt. Gideon Kaunda amesema kwa upande wao wataitumia vyema fursa ya uwekezaji katika ujenzi wa mradi huo na kuendelea kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.a

No comments: