Uhaba wa zahanati masasi

Mkuu wa gereza la Masasi,SP Juma Mgumba akisalimiana na mbunge wa jimbo la Ndanda,Cecil Mwambe alipokwenda kukabidhi msaada wa saruji na mchanga kwaajili ya ujenzi wa zahanati ya magereza.
Uhaba wa eneo la kutolea huduma za kitabibu  katika zahanati ya gereza la Masasi mkoani Mtwara huenda likapungua baada ya mbunge wa jimbo la Ndanda Cecil Mwambe kukabidhi msaada wa saruji na mchanga kwaajili ya ujenzi.

Zahanati hiyo imekuwa ikiwahudumia wagonjwa kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Masasi na kupunguza msongamano uliokuwa katika hospitali ya wilaya ya Mkomaindo.

Akizungumza mbunge huyo alisema zahanati hiyo imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa vyumba vya kutolea huduma na kufanya wauguzi kutoa huduma kwa ugumu.

" Zahanati ya magereza imekuwa msaada kwa wananchi wa wilaya ya Masasi na imekuwa ikisaidiana na ile ya Mkomaindo kutoa huduma lakini imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa vyumba vya kutolea huduma,na imani mchango nilioutoa utasaidia kujenga zahanati yetu hapa ili iwe na eneo la kutosha kutolea huduma,"alisema Mwambe
Hata hivyo alitoa msaada wa chakula kwa wafungwa wa gereza hilo.

Akizungumza mkuu wa gereza hilo,SP Juma Mgumba alisema wamekuwa wakikabiliwa na vifaa vya ujenzi wa zahanati na hivyo kulazimika kufanya kazi katika mazingira ya kujibana na kusema wana uhitaji mkubwa wa chumba cha mama na mzazi.
Alisema kuwa wanahitaji vyumba visivyopungua 14 ili kuwawezesha kutoa huduma yao kwa uzuri.

"Jeshi kama jeshi limejitosheleza lina wataalamu lakini changamoto iliyokuwepo ni ukosefu wa ujenzi wa vifaa vya zahanati kwasababu robo tatu ya watu wa Masasi hutegemea hapa na lengo letu ni kuondoa msongamano wa wagonjwa hospitali ya Mkomaindo,"alisema SP Mgumba
Akizungumza mmoja wa wagonjwa kwenye zahanati hiyo,bi Fatma Ally alisema kuwa zahanati hiyo imekuwa msaada kwao lakini bado ni ndogo na kuomba wadau wa maendeleo kujitolea michango yao ili ipanuliwe.

"Zahanati hii imekuwa ikitoa huduma kama ile ya wilaya lakini bado ni ndogo haijitoshelezi kwahiyo naomba na wadau wengine wajitolee kama alivyofanya mbunge wa Ndanda bila kujali haiko jimboni kwake,"alisema Ally
Mwisho.........

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.