FASTJET YASITISHA SAFARI KILIMANJARO-NAIROBI

Dar es Salaam, Aprili 4, 2016 -Fastjet
Tanzania imesitisha safari zake kati ya Kilimanjaro na Nairobi.
Fastjet ilikuwa  ikifanya safari kutoka Uwanja wa
Kimataifa wa Kilimanjaro kwenda Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nairobi
mara mbili kwa wiki siku za Ijumaa na Jumapaili.

Kusitishwa kwa
safari kwenye njia hiyo kunatokana na kuwepo mahitaji haba ya abiria kwenye
masoko yote mawili ya Kilimanjaro na Nairobi hali iliyosababisha kutokuwa na
manufaa kibiashara.

Shirika hilo
limeeleza kuwa  lengo lake ni kuhakikisha
linarudisha safari hizo kati ya Kilimanjaro- Nairobi pindi tu na wakati ambapo
wateja wataihitaji.
Safari za fastjet  kutoka Dar es salaam na
Kilimanjaro kwenda Nairobi zilianza Januari 11, 2016.
 Mahitaji ya abiria  kwa safari hizo  ambazo kwa kiwango kikubwa ni za kibiashara
kati ya majiji  ya Dar es Salaam na
Nairobi  ambayo kwa pamoja  yana idadi ya watu ambao ni zaidi ya milioni
nane  yamekuwa makubwa na kuifanya fastjet
hivi karibuni kuongeza safari zake
kwenye njia  hiyo  ili kukidhi mahitaji makubwa ya abiria.
Fastjet  kwa hivi sasa inafanya safari mbili za kwenda
na kurudi kati ya miji hiyo  kila siku
ndani ya wiki  na hivyo kufanya  jumla ya safari zake kwa wiki kati ya Uwanja
wa Kimataifa wa Dar es Salaam na Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta  kuwa ni 28.

 Mtiririko mpya wa safari unawapatia wateja
huduma sahihi mapema nyakati za asubuhi na
jioni  na matokeo ya ratiba hiyo  ni kuwepo kwa takribani  viti 19,000 kila mwezi kwenye safari hizo
kati ya majiji hayo mawili na hali kadhalika kuwapatia wateja  mbadala sahihi wa kusafiri kwa nauli
wanayoimudu.
Nauli za fastjet kimsingi ni za chini
ikilinganishwa na tozo za mashirika mengine ambayo kwa sasa yanafanya safari
zake kati ya Kenya na Tanzania.
Nauli  kutoka Tanzania kwenda Kenya  zinaanzia shilingi 176,000 kwa safari moja,
bila kodi ambayo ni shilingi 107,800 kwa kuondokea Tanzania  na dola 40 kwa kuondokea Kenya, na hivyo
fastjet kuwashauri abiria kukata tiketi zao mapema kabla ya siku ya kuanza
safari ili kutumia fursa hiyo ili kufaidi na nauli ya chini.
 Nauli kutoka Kenya zinaanzia dola za Marekani
120 kwa safari moja zikijumuishwa kodi za serikali ambayo ni dola 40 kwa
kuondokea Kenya.
Matokeo ya safari
hizi kati ya Nairobi na Dar es Salaam yamekuwa ni makubwa kutokana na ukweli
unaojidhihirisha kwamba nauli kwenye mashirika shindani yanayofanya safari kati
ya nchi hizi mbili zimeshuka kwa kiwango cha asilimia 40 tangu fastjet ianzishe
safari zake.
Fastjet inasisitiza kwamba  kupunguza mtiririko
wa safari kwenye njia kati ya Nairobi na Kilimanjaro kunafungua fursa  ya kuongeza uwezo zaidi kwa njia zilizopo
kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na hali kadhalika kuwepo uwezekano wa
kufungua njia nyingine mpya siku za karibuni.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.