Na Exaud Mtei
Watanzania wametakiwa
kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais DR JOHN POMBE
MAGUFULI za kupambana na ufisadi na kuleta Amani na usawa katika nchi kwani
ndio msingi wa maendeleo ya nchi yoyote duniani.
Akizungumza na wanahabari
Jijini Dar es salaam mchana wa leo kiongozi Mkuu wa chuo cha kiislam HAWZA Imam
Swadiq ambaye pia ni kiongozi mkuu wa
waislam wa dhehebu la Shia Ithnasheria nchini Tanzania SHEIKH HEMED JALALA wakati
wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa mmoja kati ya wanafuzi wa mtume ambaye ni Imam Ali aliyekuwa kiongozi jasiri kati ya wanafunzi wa mtume Mohamad amesema kuwa
Rais Magufuli ameonyesha njia ambayo Tanzania inatakiwa kuelekea hivyo ni
wakati wa watanzania kuunga mkono juhudi hizo.
Amesema kuwa Imam Ali
ambaye wanaadhimisha kuzaliwa kwake Zaidi ya miaka 1430 Alikuwa ni kiongozi
aliyepigana kuleta usawa kwa watu wote pasipo kujadi dini zao,alipinga
ufisadi,uadilifu,jambo ambalo amesema linafanana na analolifanya Rais wa Tanzania
kwa sasa hivyo ni wakati wa kumuunga mkono.
“Naweza kumfananisha
Rais wetu na kiongozi huyu Iman Ali na serikali aliyokuwa anaiongozi japo
siwezi kusema wanafanana kwa asilimia ngapi ila mambo anayoyafanya Rais Magufuli
ndiyo yale yale aliyoyafanya Imam Ali wakati akiongoza serikali”.amesema
kiongozi huyo
Aidha ameongeza kuwa
katika utawala wa Imam Ali ulisimamia sana katika kuondoa ujinga huku ukiamini
kuwa ili nchi ipate maendeleo ni lazima kufuta ujinga na kuwapa watu Elimu
jambo ambalo Rais Magufuli limekuwa kipaumbele chake hadi kuweka elimu bure
nchini ambapo amesema kuwa ni njia moja wapo kubwa na nzuri ya kuyafikia
maendeleo ya taifa.
Shekh JALALA amemaliza
kwa kwa kuwataka watanzania wote wakiwemo viongozi wa dini kuhakikisha
wamamwombe sana Rais wa Tanzania ili aweza kufanikisha lengo lake la kuifikisha
Tanzania katika mafanikio ya kimaendeleo
No comments:
Post a Comment