Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad akionesha ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015 kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo mjini Dodoma ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka 2016/2017.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo mjini Dodoma juu ya ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015 ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka 2016/2017.
Waandishi wa habari wakipokea ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015 ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka 2016/2017.
Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO
……………………………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad amekabidhi ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015 bungeni leo ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka 2016/2017.
Katika ripoti yake, CAG ametoa mapendekezo kadhaa ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi ili kuboresha matumizi ya fedha za Serikali kwa malengo yanayokusudiwa.
Miongoni mwa maeneo ambayo CAG ametoa mapendeklezo ni Ofisi ya Masjili wa Vyama vya Siasa nchini ifuatilie suala la uwasilishaji wa taarifa za fedha kwa wakati kulingana na matakwa ya sheria.
Hatua hiyo ya CAG inafuatia ukaguzi uliofanywa kwenye vyama vya siasa nchini vyenye usajili wa kudumu ambavyo jumla yao ni vyama 22.
Prof. Assad alisema kuwa kati ya vyama hivyo vyenye usajili wa kudumu, ni chama kimoja ndicho kilichowasilisha hesabu zake kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Januari hadi Juni 2015 ambacho ni Chama cha Wananchi (CUF).
Vyama vingine 21 havikuwasilisha vitabu vya hesabu kwa ajili ya ukaguzi kinyume cha kifungu Na. 14 cha Sheria ya vyama vya siasa Na. 5 ya mwaka 1992.
No comments:
Post a Comment