Mgogoro wa kisiasa
ulioibuka ndani ya chama cha upinzani nchini Tanzania cha Aliance for
democratic change ADC baina ya mwenyekiti wa chama hicho SAID MIRAAJ ABDULLA na
bodi ya wadhamini ya chama hicho mgogoro ambao umesababisha hadi mwenyekiti
huyo kusimamishwa ndani ya chama hicho
umeendelea kuchukua sura mpya baada ya viongozi wa chama hicho kuibuka
leo na kumkaanga msajili wa vyama vya siasa nchini jaji FRANSIS
MUTUNGI—anandika Exaud Mtei kutoka Dar es salaam---
Ikiwa ni miezi sita
sasa tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu nchini Tanzania ambao ulimalizika kwa
chama hicho kushindwa kufurukuta kikamilifu katika uchaguzi huo kuliibuka
sintofahamu juu ya maswala ya kisiasa ndani ya chama hicho huku mwenyekiti akituhumiwa
kutumia nafasi yake vibaya kuivuruga katiba ya chama hicho ikiwa ni pamoja na
kuwafukuza baadhi ya viongozi.
Baada ya mgogoro huo
kuonekana kukua kwa kasi hatimaye ulimfikia msajili wa vyama vya siasa nchini
ambaye kwa upande mwingine ndiye mlezi wa vyama vya siasa nchini Tanzania ambapo
aliamua kuchukua hatua mbalimbali ambazo zinaonekana kupingwa na uongozi
uliosalia ndani ya chama hicho chenye makao makuu yake Buguruni Jijini Dar es
salaam.
Akizungumza na wanahabari
leo Jijini Dar es salaam Naibu katibu mkuu wa chama hicho Doyo Hassan Doyo
ameeleza kuwa mnamo tarehe 27 mwezi wanne mwaka 2016 walipokea barua kutoka kwa
msajili wa vya vya siasa nchini inayoiagiza bodi ya wadhamini kuwa uongozi
uliochanguliwa kihalali urejeshewe mamlaka yake badala ya bodi ya wadhamini
kuchukua mamlaka ya uendeshaji wa shughuli za chama kuwa si halali,barua ambayo
wamedai inamapungufu makubwa na hawakubaliani na agizo hilo.
“Baada ya kupokea barua
hiyo tuligundua kuwa kuna mapungufu makubwa sana,kwanza haikuzingatia matakwa
ya katiba ya chama chetu zaidi ya kubeba ushabiki wa msajili na ishara ya wazi
kutaka kuuendeleza mgogoro huo ambao ulishapatiwa ufumbuzi kwa mujibiu wa
katiba ya chama,pia ilijaa upotoshaji mkubwa wa Tafsiri ya katiba yetu ya
ADC,lakini pia haina hoja zenye msingi ya kuonyesha dhamira nzuri za kumaliza
mgogoro huo” Ameeleza naibu katibu mkuu huyo ambaye naye alikuwa ametimuliwa
hapo awali na mwenyekiti wa chama hicho.
Amesema kuwa kitendo
cha msajili kutetea uongozi huo wa mwenyekiti kuendelea kuwepo madarakani
inaonyesha wazi kuwa msajili huyo ana maslahi na uongozi huo hivyo wamemtaka
kuacha mara moja kwani mwenyekiti wa chama hicho amesimamishwa kwa mujibu wa
katiba halali ya chama hicho.
Wanahabari kazini |
CHANZO CHA MGOGORO
CHATAJWA
Imekuwa ikielezwa kuwa
kumekuwa na mambo kadhaa ambayo yamesababisha mgogoro huo ndani ya ADC huku
uchaguzi wa marudio visiwani Zanziabar ukitajwa kama moja ya sababu kubwa ya
kuchochea mgogoro huo ambapo ilisemekana kuwa mwenyekiti wa chama hicho
alipingana wazi wazi na ushiriki kwa
chama chao katika uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar ambao mgombea wa chama
hicho HAMAD RASHID alishiriki na kuambulia asilimia tatu ya kura zote.
Sababu nyingine
iliyokuwa ikitajwa na baaadhi ya wachambuzi wa maswala ya kisiasa ni ile ya
mwenyekiti huyo kutumia kiti chake kuwasimamisha uanachama baadhi ya wanachama
wao akiwemo mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama hicho ambapo ndicho
kilisababisha kuongozeka kwa mgogoro huo.
Akieleza sababu za
mgogoro huo huku akikanusha sababu zote zilizokuwa zinatajwa Naibu katibu mkuu
huyo amesema kuwa sababu kubwa ya kumsimamisha mwenyekiti wa chama hicho ni
hatua yake ya kuzungumza maswala ya chama hicho mbele ya wanahabari hasa mambo
ambayo hayana Baraka ya chama hicho na mbaya Zaidi kuzungumza maswala ya kukitisha
na kukivuruga chama hicho.
“Mwenyekiti wetu
alifika mahali anamua kukivuruga chama hasa pale alipotangaza kwa wanahabari
kuwa Tarehe 11 atakifumua na kuweka mambo ya chama wazi,sisi kama viongozi wa
taasisi yenye taratibu,katiba na miongozo yake hatuwezi kusubiri kuona mtu kama
huyo akikivuruga chama na ndio sababu iliyotufanya kumsimamisha mwenyekiti
huyu.ameeleza Doyo
Ameendelea kusema kuwa
sababu nyingine ambazo zimekuwa zikitajwa kusababisha mgogoro huo ni uzushi na
uongo kwani kutofautiana mitizamo kuhusu uchaguzi wa Zanzibar hakuwezi kuleta
mgogoro kwani hayo ni maswala ya kawaida katika siasa.
Mwenyekiti wa chama hicho SAID MIRAAJ ambaye amesimamishwa na bodi ya wadhamini ya chama hicho |
TAHADHARI KWA
MWENYEKITI HUYO
Aidha katika hatua
nyingine chama hicho cha ADC kimemtaka mwenyekiti huyo kaucha kufanya mikutano
na wanahabari vichochoroni nje ya ofisi na badala yake kama anajiamini kuwa ni
mwenyekiti wa chama hicho halali ajitokeze na azungumze ndani ya ofisi zake
kwani kuendelea kuzungumza nje ya chama ni kuonyesha ni jinsi gani
anavyoichezea katiba ya chama hicho.
“Tunashangaa tunaona tu
kwenue vyombo nya habari akizungumza maswala ya chama ila hatujui anazngumzia
wapi,mwenyekiti gani anafanya mikutano yake na wanahabari nje ya ofisi
yake,kama ni mwenyekiti halali aje azungumze ndani ya ofisi za chama hapa”Ameeleza
Naibu katibu mkuu huyo.
Mwisho kabisa Naibu
katibu mkuu huyo amelitaka baraza la vyama vya siasa nchini kuacha utapeli wa
kisiasa kuwabeba viongozi ambao wana matatizo na vyama vyao ili kuepusha
migogoro isiendelee katika vyama vyao huku akiwataka wanachama na wapenzi wa
chama hicho kutulia na kuendelea kuwa na Imani na chama chao hasa kipindi hiki
cha mgogoro huu.
No comments:
Post a Comment