Saturday, April 30, 2016

MWENYEKITI WA MTAA ATAKAYESHINDA KWA KUFANYA USAFI KATIKA MTAA WAKE KUIBUKA NA MILIONI 50.000.000

????????????????????????????????????
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiongozana na Mwanamuziki Diamond Plutnamz pamoja na Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti Clods FM Bw. Ruge Mutahaba wakati wa matembezi ya mshikamano kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya usafi wa jiji la Dar es salaam itakayofanyika kwa siku 90 ikishirikisha wenyeviti wa mitaa,  wananchi katika maeneo yao, Taasisi za Serikali na Mashirika Binafsi ili kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakuwa safi kabisa.
Makonda amewaambia wananchi mara baada ya matembezi hayo kwamba Dar es salaam bila uchafu inawezekana na amenzisha shindano kwa wenyeviti wa mitaa iliyopangwa na isiyopangwa mwenyekiti atakayeshinda kwa usafi katika eneo lake atajishindia shilingi milini 50.000.000 na mwenyekiti atakayekuwa wa mwisho katika eneo lake atapata nafasi ya kutangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na uchafu uliopo katika eneo lake na wananchi wake na pia mazingira hayo machafu yataonyeshwa yakiambatana na picha za mwenyekiti huyo.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi na Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti Radio Clods Bw. Ruge Mutahaba na Mwanamitindo Millen Magesse ambaye pia ameshiriki kikamilifu katika kampeni hiyo
????????????????????????????????????
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi na Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti Radio Clods Bw. Ruge Mutahaba na Mwanamitindo Millen Magesse ambaye pia ameshiriki kikamilifu katika kampeni hiyo
????????????????????????????????????
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiongozana na Diamond Plutnamz huku ulinzi ukiwa umeimarishwa wakati wa matembezi hayo yaliyofanyika leo kwa ajili ya kuhamasisha wakazi wa jiji la Dar es salaam kufanya usafi katika maeneo yao.????????????????????????????????????Haya ni miongozi mwa matukio yaliyojiri wakati wa matembezi hayo ya kuhamashiwa wakazi wa jiji kufanya usaifi ambapo kampeni maalum ya siku 90 za kufanya usafi zimezinduliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Wapiga picha waliendelea na ubunifu wa kutafuta picha nzuri kama wanavyoonekana hapa kwenye picha wakiwa kwenye pikipiki wakipiga picha katika matembezi hayo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya washiriki wa matembezi hayo wakifanya mazoezi mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam ambako ndiko kampeni hiyo ilikozinduliwa.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akishiriki katika mazoezi hayo mara baada ya mtembezi hayo kuwasili katika viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akisalimiana na viongozi wa dini waliofika katika uzinduzi wa kampeni hiyo ambao ni Sheikh Mkuu wa Dar es salaam Sheikh  Alhadi Mussa Salim na  Askofu  David  Mwasota kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally  Hapi????????????????????????????????????Kikundicha ngoma kikitumbuia katika uzinduzi huo
12Kundi la Yamoto Band likitumbuiza katika zunduzi huo.
13
14Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo wakiwa katika viwanja vya Leaders Kinondoni.
15Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh. Sophia Mjema, Askofu David Mwasota, Sheikh Mkuu wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi wakiwa katika uzinduzi huo.
16Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika kwenye viwanja vya Leaders mara baada ya matembezi ya kuhamasisha wananchi kufanya usafi katika maeneo yao.
IMG_6078Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam wa pili kutoka kushoto na wenyeviti wa wenyeviti wa mitaa kutoka wilaya zote tatu wakifanya ishara ya kufangia ikiwa ni uzinduzi rasmi wa siku 90 za kufanya usafi katika jiji la Dar es salaam kutoka kulia ni Juma Ngemwa Kinondoni, Mbayo Chuma Ilala na Bakiri Makere Temeke.
IMG_6086Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi akizungumza katika uzinduzi huo na kutoa maagizo kwa watendaji na watumishi wa Manispaa ya Kinondoni kuhakikisha wanazingatia na kutimiza malengo kuhakikisha Kinondoni inakuwa safi.

No comments: