Tuesday, May 3, 2016

MAADHIMISHO YA KUZALIWA KWA ACT-Wazalendo



Tarehe 05 Mei, 2016 Chama cha ACT Wazalendo kitaadhimisha miaka miwili ya kuzaliwa kwake. Kitaifa, maadhimisho haya yatafanyika wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani mgeni rasmi katika maadhimisho haya atakuwa  Mwenyekiti wa Chama Taifa Mama Anna Mghwira.


Mwenyekiti wa Taifa Mama Anna Mghwira ataambatana na  Kaimu Katibu Mkuu Ndugu Juma Sanani pamoja na  viongozi wengine wa  kitaifa.

Katika maadhimisho hayo Mwenyekiti wa Chama Taifa atazindua matawi mapya zaidi ya ishirini, kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii na baadaye kuhutubia mkutano wa hadhara Mkuranga Mjini.

Kwa upande wa Zanzibar, Maadhimisho haya  yataenda pamoja na wanachama na viongozi wa ACT Wazalendo kujitolea damu kwenye Benki ya Damu Zanzibar na kutoa misaada mbalimbali kwenye kituo cha Wazee cha Barazani  “Barazani kwa Wazee”.

Kwa sasa shamra shamra za maadhimisho haya yanafanyika pia kwenye mikoa yote nchini kwa viongozi na wanachama wa ACT-Wazalendo kushiriki katika shughuli za kijamii kabla ya siku ya hitimisho yake Alhamis Mei 5.

Abdallah Khamis,
Afisa Habari
ACT Wazalendo
Imetolewa leo tarehe 03 Mei, 2016

No comments: