Monday, May 30, 2016

Maoni kutoka kwa wanasiasa mbalImbali kuhusu kilichojiri bungeni leo

Nimekukusanyia baadhi ya maoni mbalimbali ya wadau na viongozi wa kisiasa nchini kuhusu kilichojiri bungeni na kauli zao,Hapa ninaye Katibu mkuu wa chama cha ADC,ndugu DOYO HASSAN DOYO ninaye pia mwanasiasa na mwanachama wa CUF na mchambuzi wa siasa JULIUS MTATIRO na mwanaharakari MALISA GODLISEN

DOYO HASSAN DOYO-----Nimepokea taarifa kuwa wabunge vijana mmoja wa chadema na mmoja WA act wazalendo, yaan mh, zito kabwe, na mh Halima mdee wamefungiwa kushiriki shughuli za bunge mpaka mwezi wa tisa, Huu ni hujuma dhidi ya TAIFA letu kuhusu kudai haki, ndani ya vyombo husika, pia nimepata taarifa wabunge wengine mh, tundu lissu na Ester bulaya wamesimamishwa, kitendo hiki ndyo maono ya serikali ya awamu ya tano Namna ambavyo imejiandaa kuminya democrasia ndani ya Nchi yetu, kwa kitendo hicho tunajianda na mapambano haya ambayo ukomo wake ni pale tutakapo pata fursa za kweli za kuzungumza ukweli ndani ya Nchi yetu,
MTATIRO J----Tundu Lissu na Esther Bulaya wafungiwa kuhudhuria vikao vyote vilivyobaki vya bunge la bajeti na bunge lijalo la mwezi wa tisa. (Kwa hiyo hawatarudi bungeni hadi mwaka 2017).

Zitto Kabwe, Pauline Gekul, Godbless Lema na Halima Mdee wamefungiwa kushiriki vikao vilivyobaki vya bajeti na John Heche amefumgiwa kuhudhuria vikao kumi mfululizo vya bajeti kuanzia leo. (Watarudi bungeni Septemba).

Huu ni uamuzi wa kamati Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge chini Mh. George Mkuchika (Mb). Asilimia 80 ya wabunge wa Kamati hii ni wana CCM.

                                             MY TAKE;
                                 Huu  ni ujinga wa KARNE!
Africa do need strong institution and not strong people. HAPA UDIKTETA TU, WAMESHATUMBULIWA.....TUNAISOMA NAMBA!


MALISA------Nchi hii ina matatizo mengi. Sukari, ajira, elimu, maradhi, Ujinga, Umasikini etc. Lakini tatizo kubwa zaidi kwa sasa ni Naibu Spika. Ni unyama kukataa mjadala kuhusu watoto wanyonge wa maskini waliofukuzwa usiku wa manane bila kuambiwa hatma yao ili tu kulinda maslahi ya chama chako. Dhambi kuu.!

"Tumesimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge, hatuko tayari kuwa sehemu ya kupitisha maamuzi ya hovyo na kupiga mihuri maamuzi ya kunajisi nchi yetu tutakua tayari kwa adhabu yoyote bila kuogopa".-John Heche

Ridhiwani Kikwete " lazima ifike sehemu adabu itawale Bungeni. Hawa wabunge wamepewa kitu wanachostahili. Kanuni zimetendewa haki. Naunga hoja mkono".

No comments: