Tuesday, May 31, 2016

SERIKALI KUANZISHA BAENKI YA MAENDELEO YA VIWANDA NCHINI.

MSRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua nembo mpya ya Tuzo za Rais kwa Wazalishaji bora wa Viwanda  PMAYA The President’s Manufacure of the Year  pamoja na Mwenyekiti wa Wenyeviwanda Tanzania CTI Dkt. Samwel Nyantahe katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU / HASSAN SILAYO-MAELEZO
MS2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wadau mbalimbali wa CTI na kutoka Sekta ya Viwanda nchini kabla ya kutoa Tuzo za Rais kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka 2015 katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.
MS3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini Leodgar Tenga mara baada ya kumalizika kwa hafla hio ya utoaji Tuzo za Rais.
MS4Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya Wadau wa Viwanda nchi mara baada ya kumalizika kwa hafla hio ya utoaji Tuzo za Rais.
WAF1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia na Waziri wa Nishati na Madini wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.

WAF3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea baadhi ya mabanda ya bidhaa zinazotoka viwandani wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
WAF4Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akiongea na wadau wa sekta ya Viwanda wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 na kuwataka kuunganisha nguvu katika uanzishaji na uendelezaji wa viwanda nchini ili kuongeza upatikanaji wa bidhaa nchini hali itakayopelekea kukuza uchumi wa nchi na kuongeza ajira kwa watanzania.
WAF5Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua nembo ya shirikisho la viwanda nchini wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTILeodger Tenga na wa pili ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki wa Viwanda nchini Tanzania (CTI)Dr.Samuel Nyantahe.
WAF6Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wadau wa sekta ya viwanda nchini(hawapo pichani) na kuwaahidi kuwaunga mkono katika harakati za kuendeleza sekta ya viwanda ikiwamo kuanzisha banki ya maendeleo ya viwanda nchini itakayosaidia kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wale wenye nia ya kuanzisha viwanda.
WAF7Wadau wa Sekta ya Viwanda nchini wakimsilkiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
WAF8Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa tuzo kwa washindi wa tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
WAF9Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa tuzo kwa washindi wa tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
WAF10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.                                Lilian Lundo-MAELEZO







Serikali ya awamu ta Tano imedhamiria kuifanya sekta ya Viwanda nchini kuchangia pato la taifa kwa asilimia 40 ifikapo mwaka 2020 kutoka asilimia 7.3 ya sasa
Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli amesema kuwa jambo hilo linawezekana hasa kwa kuzingatia nchi yetu ina rasilimali zinazohitajika katika kujenga uchumi wa viwanda.
“Nafahamu kwamba tunakila aina ya rasilimali inayowezesha uwepo wa viwanda hapa nchini ikiwemo umeme wa kutosha pamoja na malighafi zake na kwa maana hiyo serikali ya awamu ya tano imepanga kuifanya sekta ya viwanda kuchangia pato la taifa kwa asilimia 40 ifikapo mwaka 2020 kutoka 7.3 ya sasa”. Alisema Rais Magufuli.

Aidha Dkt. Magufuli aliwatoa wasiwasi wadau hao kuhusu uwepo wa soko la uhakika kwa bidhaa zitakazozalishwa kwani Tanzania imezungukwa na nchi zenye uhitaji wa bidhaa mbalimbali na pia ni Mwanachama wa jumuiya mbalimbali ndani na nje ya Afrika.
Naye Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage aliwataka wamiliki wa Viwanda Nchini kuunganisha nguvu katika uanzishaji na uendelezaji wa viwanda nchini ili kuongeza upatikanaji wa bidhaa nchini hali itakayopelekea kukuza uchumi wa nchi na kuongeza ajira kwa watanzania.

No comments: