SHEIKH JALALA-MAARIFA YANAPATIKANA KWENYE VITABU MBALIMBALI TUSOME

Sheikh JALALA akifungua Rasmi maktaba ya vitabu vya mafunzidho mbalimbali ya kidini Iliyopo jijini Dar es salaam yenye lengo la kuwasaidia waumini wa Dini mbalimbali katika kupata mafunzo ya dini zao
 Vijana nchini Tanzania wametakiwa kujijengea utaratibu wa kujisomea vitabu mbalimbali vya dini ili waweze kujua ni jinsi gani watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini waliishi kwa Amani na njia za kuweka maelewano katika jamii.

Wito huo umetolewa Jijini Dar es salaam na Shekh Mkuu wa madhehebu ya SHIA nchini Tanzania Sheikh HEMED JALALA wakati akifungua rasmi maktaba mpya iliyopo Jijini Dar es salaam yenye vitabu ya mafubdisho mbalimbali ya dini zote.Amesema kuwa makatba hiyo imekuja kwa ajili ya kuwasaidia vijana na watanzania mbalimbali bila kujali Itikadi zao za kidini katika kupata mafundisho mbalimbali yatakayowasaidia kuwatoa katika matatizo mengi yanayowakabili katika jamii.

Ameongeza kuwa vijana wa Tanzania ndio nguvu kazi ya taifa hivyo maktaba hiyo imekuja kwa ajili ya kuwaelekeza ni jinsi gani wanaweza kuwa tegemeo katika taifa la Tanzania na kuachana na changamoto mbalimbali zinazowakabili zikiwemo za utumiaji wa madawa ya kulevya ambazo zimezidi kukithiri katika taifa kwa sasa.Sheikh JALALA ameeleza kuwa kijana yoyote anayehitaji kuwa na uelewa mkubwa wa maswala ya Amani na dini ni lazima aitafute elimu katika vitabu mbalimbali vilivyoandikwa na viongozi wakubwa jambo ambalo ameeleza kuwa maktaba hiyo imekuja mahususi kwa ajili ya kuwasaidia watanzania kuleta maelewano,Amani,na masikilizano kwa jamii yote.Ufunguzi wa maktaba hiyo Jijini Dar es salaam umekwenda sambamba na maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa imam na kiongozi wa 12 baada ta mtume ambaye alikuwa katika mstari wa mbele katika kuahamasisha umoja,maelewano,masikilizano duniani ambapo ameongeza kuwa maktaba hiyo pia itatumika kuwapa nafasi watu kusoma mafunzo mbalimbali ya kiongozi huyo.About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.