Catherine Tundaraza Moja kati ya wanafunzi walioshiriki katika Warsha hiyo akichangia maswala mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa na wataalamu hao leo |
Na Exaud Mtei Dar es
salaam-0712098645
Wakati dunia na Tanzania
kwa ujumla ikiwa katika harakati za kumkomboa mtoto wa kike hususani katika
haki zake ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa sera ya 50/50 inafikiwa,bado Tanzania
imetajwa kuwa na chanamoto nyingi zinazomgusa mtoto wa kike huku serikali
ikitakiwa kutekeleza kwa vitendo swala la kumpatia mtoto wa kike haki sawa.
Moja kati ya mambo
ambayo yanatizamwa kama changamoto kubwa kwa sasa ni swala la ndoa na sheria ya
ndoa nchini ambayo imekuwa katika mikanganyiko mikubwa baina ya wadau wa
maswala ya haki za binadamu ambapo sheria hiyo imekuwa ikiruhusu mtoto wa miaka
14 kuolewa huku sheria ya mtoto nchini ikielekeza kuwa mtoto chini ya miaka 18
haruhusiwi kuolewa jambo ambalo limekuwa likipigiwa kelele na wadau mbalimbali
wakitaka mabadiliko ya haraka ya sheria hiyo.
Kutokana na maswala
mbalimbali yanayowakumbva watoto wa kike nchini hususani wanafunzi na wale
waishio vijijini kukosa elimu mahususi kuhusu maswala hayo wadau mbalimbali
yakiwemo mashirika ya umma na binafsi yamekuwa yakijitolea kufanya makongamano
mbalimbali kuwakutanisha watoto wa kike na kuweza kuzungumza nao na kuwapa
elimu juu ya haki na wajibu wa mwanamke katika jamii.
Shirika la WOMEN ACTION
TOWARDS ECONOMIC DEVELOPMENT (WATED) wameendesha warsha ya siku moja kwa
kuwakutanisha wanafunzi wa shule mbalimbali Jijini Dar es salaam hususani
watoto wa kike lengo likiwa ni kuinua uelewa wa wanafunzi hao juu ya haki zao
kama watoto wa kike na jinsi gani ya kukabiliana na changamoto mbalimbali
zinazowakumba katika mazingira yao.
Katibu wa WATED Tanzania MARIA MATUI akiangumza na wanahabari nje ya warsha hiyo Lep Jijini Dar es salaam |
MARIA MATUI ni katibu
wa WATED nchini Tanzania ameueleza mtandao huu kuwa lengo kubwa la
kuwakutanisha wasichana na wanafunzi wa shule za Dar es salaam ni malengo makuu
ya shirika lao kuhakikisha kuwa wanamwelimisha mtoto wa kike na ndicho
wanachokifanya kila siku katika shirika lao.
“Leo tumewakutanisha
wanafunzi mbalimbali wa shule za secondary Jijini dar es salaam ambapo
watakutana na wataalam na wanataaluma wa kada mbalimbali wakiwemo wa maswala ya
sayansi na Technologia,wataalamu wa sheria na watu wa ustawi wa jamii lengo ni
kuzungumza na watoto wa kike ambao ndio Taifa linalotegemewa waweze kujitambua
na kutambua haki zao pamoja na kufahamu nini cha kufanya katika masomo yao ili
waweze kufanikiwa”Amesema MARIA MATUI.
Ameongeza kuwa lengo
kubwa la kufanya warsha hizo hasa kwa mtoto wa kike na sio wa kiume ni ukweli
kwamba katika jamii zetu pamoja na kwamba changamoto za kimaisha ni za wote
lakini ni ukweli usiopingika kuwa mtoto wa kike amekuwa akikumbana na
changamaoto nyingi Zaidi hivyo wameona waanze na kundi hilo.
Mtandao huu umezumza na
baadhi ya wanafunzi ambao walifanikiwa kushiriki katika warsha hiyo ambapo
CATHERINE TUNDARAZA na FLORA JOSEPH wa
shule ya kisutu Jijini Dar es salaam wameeleza furaha yao baada ya kupatiwa
elimu hiyo muhimu kwa mtoto wa kike wa sasa huku wakiwasihi wahusika
kuhakikisha kuwa wanawafikia watoto wengi Zaidi hususani wa vijijini kwani ndio
wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi Zaidi kulingana na mazingira
wanayoishi.
No comments:
Post a Comment