Friday, May 6, 2016

Yaliyojiri katika ufunguzi wa TSN Hypermarket Rock City Mall, Mwanza.

 Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage akikata utepe kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa TSN Hypermarket Rock City Mall, Mwanza.
 WAKAZI wa Mwanza wajidai, TSN imefungua Hypermarket mbayo ni tawi jingine jipya la TSN mjini Mwanza, Hypermarket hii inayoendelea kutoa huduma kwa wakazi wa Mwanza imefunguliwa kuwafikia wakazi wa Mwanza waliokuwa wakikosa uhondo wa bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu zikiwemo mbogamboga fresh kutoka hapa hapa nyumbani.
Akizungumza katika ufunguzi huo Mkurugenzi wa TSN Farough Baghozah alisema... Tanzania Sisi Nyumbani - TSN mteja ni haki yake kupata kilichobora katika kiwango cha kimataifa.

"Hii ni hatua nyingine kubwa ya kuhakikisha Watanzania wanapata vitu fresh.. kutoka nyumbani. .tena kwa bei nafuu...TSN tunahakikisha Watanzania wanafurahia mazao yao wenyewe...tena kwa bei ya gengeni katika Hypermarket hii.... karibuni sana TSN Hypermarket Mwanza." alisema. 
Naye waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi huo aliipongeza hatua iliyochukuliwa na TSN katika kuthamini mchango wa wawekezaji wa nyumbani. .PICHA NYINGINE ZA TUKIO HILO BOFYA CHINI











No comments: