DUNIA TUUNGANE KUWATETEA WAPALESTINA WANATESEKA-SHEIKH JALALA

Kiongozi Mkuu wa kiroho wa Waislam Dhehebu la SHIA ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA (Katikati) akifafanua jambo kuhusu maswala ya mateso na dhuluma yanayoendelea kurepotiwa kutoka nchi ya palestina ambapo amewataka watanzania na dunia kwa ujumla kuungana kwa pamoja kuhakikisha kuwa wanawatetea wananchi wa Palestina wanaonyanganywa haki yao ya kukaa kwa amani katika nchi yao

Na Exaud Mtei (Dar es salaam)
Wakati report za mateso na dhuluma zikiendelea kurepotiwa duniani zikiyahusisha mataifa ya pelestina na israel ambapo taarifa zimekuwa zikendelea kuonyesha jinsi Taifa la palestina wananchi wake wanavyopata mateso kutoka kwa taifa la israeli hatimaye  Kiongozi Mkuu wa kiroho wa Waislam Dhehebu la SHIA ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA ameibuka na kuvitaka vyombo husika vikimeno umoja wa nchi za ulaya,umoja wa nchi za Africa,umoja wa nchi za kiarabu na dunia nzima kwa ujumla kuonyesha dhamira ya dhati ya kulisaidia Taifa la palestina na kuondokana na mateso wanayoyapata kutoka kwa taifa la Israeli mateso ambayo yamekuwa yakiendelea kwa  miaka mingi sasa.
Sheikh JALALA akizungumza na wanahabari mapema leo Jijini Dar es salaam ikiwa ni kuelekea uazimisha siku ya QUDS duniani ambayo ni siku maalum ya kukumbuka mateso wanayokumbana nayo wananchi wa palestina amesema kuwa imefikia wakati sasa dunia kwa pamoja kuungana bila kujali Dini na itikadi zake na kupigania haki ya wapalestina kwani wanaoteseka kule sio waislam pekee bali ni wananchi wote na hata wale wasio na dini.


Akieleza sakata linaloendelea katika nchi hiyo ya palestina amesema kuwa mateso yamekuwa yakiongezeka kadiri siku zinavyosogea ikiwa ni pamoja na nyumba za wananchi kuvunjwa,makanisa na misikiti kuharibiwa,mauaji ya kila kona,na kuharibiwa kwa mashamba yao ambayo wamekuwa wakulima wa mazao ya mizaituni jambo ambalo amesema kuwa linaonyesha wazi ni mipango ya wazi ya kuwamaliza wapalestina na kuwaondoa kabisa katika ardhi yao jambo ambalo amesema halifai kunyamaziwa na walimwengu wote.
Profesa ABDUL SHARIFU ni mstafu wa chuo kikuu cha Dar es salaam ambapo katika mkutano huo na wahabari naye alipata nafasi ya kueleza chanzo cha mgogoro kati ya mataifa hayo mawili na jinsi gani kwa sasa unaathiri maisha ya wana palestina kwa ujumla
Ameogeza kuwa mkakati uliopo hapo kwa sasa ni mkakati wa kufutwa kabisa kwa upalestina na kuwaondoa kabisa katika ardhi yao na katika nchi yao wakati ni wazi kwa nchi hiyo ni nchi yao halali na wanastahili kuishi kwa Amani kama mataifa mengine.
Akielezea jinsi dunia inavyotakiwa kuungana amesema kuwa katika kuwapigania wapelestina waweze kupata Amani yao sio maswala ya kidini wala kiitikadi bali ni jambo la kibinadamu ambalo halina dini wala kabila na ni jambo la utu la kutetea haki za wanadamu wenzetu ambao wanateseka mikononi mwa waisrael.
Pamoja na wito huo na kilio cha SHEIK JALALA pia ametoa wito kwa watanzania wote wakiwemo viongozi wan chi  kutokana na historia nzuri iliyopo tangu kipindi cha baba wa Taifa Mwalimu NYERERE la kuwa taifa lenye  mahusiano mazuri kwa wapalestina amelitaka taifa kufwata nyayo za Baba wa taifa na kuamua kuwasemea wapalestina na kuhakikisha kuwa wanapata haki yao wanayostahili.
NICE MUNISI ni mmoja kati ya watanzania wachache waliowahi kunafya ziara katikia nchi ya palestina na kujionea ukubwa wa mgogoro huo ambapo hapa akisimumua ushughuda wake kuhusu yale aliyojionea nchini palestina ambapo amesema kuwa alichokiona ni mateso makubwa sana wanayokumbana nayo wananchi wa palestina na dhuluma kubwa kutoka kwa Taifa la ISRAEL hivyo akaendelea kuunga mkono Juhudi za kuunganisha dunia ili kuwatetea wananchi hao amabo hawana hatia lakini wanakumbana na mateso makubwa
Katika kuonyesha kukerwa na maswala yanayoendelea nchini palestina Sheikh JALALA amewataka watanzania wote kwa ujumla kutoka kwa umoja wao siku ya ijumaa ya tarehe 1,mwezi wa Saba kufanya matembezi ya Amani ya kuonyesha dunia kuwa watanzania tunapinga kwa pamoja dhuluma wanayofanyiwa wapalestina katika ardhi yao matembezi ambayo yatafanyika katika Jiji la Dar es salaam.

Mgogoro wa Mataifa ya palestina na Irael ni mgogoro mkubwa ambao kwa sasa umechukua miaka mingi na umekuwa ukikuwa mwaka hadi mwaka huku taifa la palestina likionekana kuumizwa Zaidi na mgogoro huo kutokana na madhara makubwa yanayowakumba wananchi wake likiwemo wananchi kuuawa,wengine kukosa makazi pamoja na maelefu ya wananchi wa palestina kufungwa katika magereza ya Israeli kwa sababu ambazo sheikh JALALA amezitaja kuwa hazina mashiko.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.