SHEIKH JALALA AONGOZA MAMIA KATIKA MATEMBEZI YA AMANI KUWATETEA WAPALESTINA JIJINI DAR ES SALAAM

Mamia ya wakazi wa Jiji La Dar es salaam leo wamejitokeza kwa wingi wakiongozwa na Kiongozi Mkuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la Shia ITHNASHERIYA TanzaniaSheikh HEMED JALALA wamejitokeza kwa wingi katika mitaa ya Dar es salaam kufanya matembezi ya amani kulaani vikali matendo ya unyanyasaji na ukandamizwaji unaoendelea katika nchi ya palestina ikiwa leo ilikuwa ni maadhimisho ya siku ya QUDS Duniani ambayo ni siku ya kukumbuka na kupaza sauti kulaani matendo maovu yanayofanywaq juu ya wanadamu wa Taifa la palestina matendo ambayo yamekuwa yakifanywa na Taifa la ISRAEL.Kiongozi Mkuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la Shia ITHNASHERIYA TanzaniaSheikh HEMED JALALA akizngumza na wanahabari leo wakati wa matembezi hayo ambayo yalianzia katika shule ya msingi ilala Boma na kumalizikia kigogo ambapo amesema kuwa huu ni wakati wa mataifa yote yanayopenda amani likiwemo Taifa la Tanzania kupaza sauti zao kwa pamoja kulaani na kukemea yale ambayo yanatokea palestina kwa sasa kwani watu wamekuwa wakipata mateso ambayo kimsingi yanahitaji msaada wa kutoka nje ili kukomesha matendo hayo.
.
Sheikh JALALA amesema kuwa matembezii hayo ambayo yamefanyika ikiwa ni ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ni ishara ya kukerwa na kulaani vikali yanayotokea Palestina kwa sababu watu wanaoteseka kule ni wanadamu wa aina mbalimbali wa dini zote hivyo kuwatetea ni jukumu la kila mwanadamu bila kujali itikadi zozote
Wa kwanza kushoto ni Kiongozi Mkuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la Shia ITHNASHERIYA TanzaniaSheikh HEMED JALALA akiongoza mamia ya wananchi na waumini wa Dini ya kiislam katika matembezi hayo ambayo yalitumika kama ishara ya kuionyesha Dunia yale ambayo yanatokea nchini palestina.PICHA NYINGINE ZA MATEMBEZI HAYO ZIPO HAPO CHINI----------

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.