Friday, July 1, 2016

TWCC WAIBUKA NA TUZO HII UFUNGUZI WA MAONYESHO YA SABA SABA LEO

Bi. Jaqueline Mneney Maleko ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha TANZANIA WOMEN CHEMBER OF COMMERCE (TWCC) akionyesha Tuzo yao waliyoipata leo katika siku ya ufunguzi wa maonyesho ya siku ya saba saba Jijini Dar es salaam
Na VICENT MACHA Dar es salaam

Chama cha TANZANIA WOMEN CHEMBER OF COMMERCE(TWCC)kimetunikuwa  tuzo ya taasisi bora inazowezesha ukuwaji wa biashara katika kinya n’ganyiro cha saba katika vinyanganyiro Zaidi ya 18 vilivyokuwa vikigombaniwa katika maonyesho ya saba saba yaliyozinduliwa leo na Rais wa Rwanda Mh PAUL KAGAME.

Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu katika maonyesho hayo Bi. Jacqueline Mneney Maleko ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho  amesema tuzo hiyo ni chachu kwa TWCC kuweza kuongeza juhudi katika kutimiza wajibu wao na ni kwa mwaka wa kwanza tangu achaguliwe kuwa mwenyekiti na kuwezesha kupata tuzo hiyo.
Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa  kutokana na vigezo walivyokuwa wakitumia kupata washindi hao ni pamoja na  kuangalia ubora wa bidhaa na  kuwahoji maswali wauzaji au watengenezaji wa bidhaa hizo na pia hawakuwa na wasi wasi na kinyan’ganyiro hicho kwa kuwa walijiandaa vya kutosha na walihakikisha wanaweza kushinda kutokana na maandalizo hayo makubwa.

Aidha mwenyekiti huyo amempongeza Bi KONSOLATA ambaye ni mwanamke pekee ambaye aliweza kuchimba madini na pia kuyachonga jambo ambalo limekuwa nadra sana kwa wanawake wa kitanzania kufanya na imezoeleka kufanywa na wanaume pekee lakini kwa Mwanamke huyo ni Tofauti sana.

 KONSOLATA alikuwa ni miongoni mwa watu walioweza kuhojiwa na Mtandao huu ambapo amesema kuwa kitu kilichoweza kuwapa ushindi ni umoja walio nao wana TWCC wote na pia TWCC iliweza kuwafundisha kukabiliana na masoko ya kimataifa hivyo ni mbinu hizo zimewafanya kuweza kuibuka washindi.

Maonyesho ya saba saba yamezinduliwa leo na Rais wa Rwanda Mh PAUL KAGAME na Mwenyeji wake Mh Rais MAGUFULI ambapo yakamalizika siku ya Tarehe saba ambapo ni kilele cha siku ya Sabasaba Huku TWCC wakiwa ni moja kati ya wafanya biashara wanaoshirika katika maonyesho hayo.



No comments: