Tuesday, July 26, 2016

ZITTO AWASILI MAREKANI

 Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Ndugu Zitto Kabwe akiwa na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad,Katika Mkutano Maalum wa Viongozi wa Kisiasa Ulimwenguni (International Leaders Forum) ambao Unafanyika Leo Asubuhi (Kwa Saa Za Marekani) Jijini Philadelphia.

Mkutano huo ulioandaliwa Na Asasi ya NDI (National Democratic Institute), Ni Sehemu ya Matukio Maalum kuelekea Mkutano Mkuu wa Chama Cha Democrats (Democratic National Convention), Mkutano ambao utamthibitisha Bibi Hillary Clinton Kuwa Mgombea Urais Kupitia Chama Hicho.
Zitto Kabwe Pamoja Na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim watakuwa Philadelphia mpaka Siku ya Alhamis ambapo  Mkutano huo unategemewa kumuidhinisha Bi Hillary Clinton Kuwa Mgombea Urais wa Marekani kupitia Chama Hicho.
Abdallah Khamis
Afisa Habari, ACT Wazalendo



No comments: