TGNP YAWAPIKA WANAHABARI TANZANIA JUU YA BAJETI YENYE MLENGO WA JINSIA

Mkurugenzi wa mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP akizungumza na wanahbari leo Jijini Dar es salaam katika makao makuu ya Mtanzdao huo wakati akizindua Warsha ya siku mbili kwa wanahabari iliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo wanahabari jinsi ya kureport Habari za jinsia Hususani Kujadili kwa kina Bajeti ya Tanzania na jinsi Gani inaweza kuwa katika mlengo wa jinsia.

Wakati akizindua warsha hiyo amewataka wanahabari kuhakikisha kuwa wanaijadili na kuizungumza Bajeti ya Tanzania katika mlengo wa Jinsia ili iweze kusaidia Jamii kwa mapana yake.

Wanahabari mbalimbali Kutoka katika vyombo vya habari nchini wakiwa wanafwatilia kwa makini Warsha hiyo iliyoandaliwa na mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP leo ambapo ilikuwa ni semina maalum ya kuwajengea uwezo wanahabari juu ya Kureport Bajeti yenye mlengo wa Jinsia nchini Tanzania na Utekelezaji wake

Deogrtius Temba Mjumbe kutoka Mtandao wa jinsia Tanzania TGNP akiwa anawasilisha mada mbalimbali katika warsha hiyo leo jijini Dar es salaam

Moja kati ya wanahabari waliopata nafasi ya kuhudhuria Warsha hiyo ni mwanahabari mahiri kutoka Kituo cha TV cha ITV Pichani akichangia mijadala mbalimbali juu ya jinsi Gani wanahabari wanaweza kuisaidia jamii kwa kuhakikisha kuwa wanareport Habari za bajeti katika mlengo wa kijsia jambo ambalo limetajwa litasaidia katika kuleta usawa katika jamii hususani katika kutumia Bajeti ya Tanzania ambayo imekwisha pita.
REPORT KWA VIDEO UNGANA NA HABARI24 TV YOUTUBE 

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.