MBEYA CITY FC YAIWINDA MBAO FC

t
IMG-20160830-WA0024IKIWA inaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao Fc  uliopangwa kuchezwa mwishoni mwa juma hili kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mbeya City fc  inataraji kuondoka mjini Shinyanga   ijumaa hii kuelekea jijini Mwanza  tayari kwa  kuikabili timu hiyo  iliyopanda daraja  kwa ‘mtereko’ tiketi ya mezani.
Mapema  leo kwenye uwanja wa Kambarage  wakati wa mazoezi ya asubuhi  afisa habari wa kikosi hiki, Dismas Ten,  amesema kuwa  City  itaondoka  mjini Shinyanga  ijumaa  jioni kuelekea  jijini Mwanza  ikiwa na lengo moja tu la kuvuna  pointi tatu zingine  kwenye uwanja wa CCM Kirumba  kama  ilivyokuwa kwenye mchezo wa juma lililopita dhidi ya wenyeji Toto Africans.
“Tumekuwa hapa Shinyanga  toka siku ya jumatatu, kwa ajili  ya mazoezi na matayarisho ya mchezo wa jumamosi,Mwalimu alichagua  kufanya mazoezi Kambarage  kwa lengo moja tu la kupata utulivu na kuandaa kikosi vizuri ili kuhakikisha tuanshinda  na kupata pointi tatu kwenye siku nzuri ya Septemba 3 , kikosi chetu kiko sawa, pasipo majeruhi yeyote na tunakwenda Mwanza kucheza kwenye uwanja ambao  siku zote tumekuwa na bahati nao”. alisema
IMG-20160830-WA0023Akiendelea  zaidi Ten aliweka wazi kuwa kiungo Geoffrey Mlawa  na mshambuliaji Omary Ramadhani waliyopata majeraha  kwenye mchezo uliopita  dhidi ya Toto Africans wamerejea kwenye hali  nzuri  na anaweza kuwa  sehemu ya mchezo huo wa jumamosi endapo Mwalimu Kinnah Phiri  atapenda kuwatumia.
“Dakika 90 zilizopita tulizihitimisha kwa kupata majeruhi wawili kwa Omary Ramadhani na Geoffrey Mlawa, jopo la madaktari  wamethibitisha kuwa  wachezaji hao wako sawa na wanaweza kucheza kwenye mchezo wa jumamosi ingawa jambo hilo  litategemea  na  maamuzi ya mwalimu, kuwepo kwao kikosini  kutaongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji ambalo ni muhimu kwenye kusaka pointi tatu,hasa ukizingatia kiwango kizuri walichokionyesha kwenye mechi dhidi ya Toto Africans” alimaliza.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.