ACT-WAZALENDO WASOGEZA MBELE MKUTANO WAKE,HII NDIYO TAREHE RASMI,NA SABABU ZAO

1.    Katika kikao chake cha tarehe 05 Septemba 2016, pamoja na mambo mengine, Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo iliazimia kuwa Chama kifanye Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia (National Democratic Congress) tarehe 24 Septemba 2016 jijini Dar es Salaam.
  2Tangu kutangazwa kwa umma kuhusu mipango ya kufanyika kwa mkutano huu, wanachama wetu wengi na wananchi kwa ujumla, wakiwemo baadhi kutoka mikoani wameonesha nia ya kushiriki. Ili kuwapa fursa viongozi, wanachama na wananchi kushiriki kwenye mkutano huu, Chama kimesogeza mbele tarehe ya kufanyika kwake hadi tarehe 08 Octoba 2016.


3.    Wanachama na wananchi ambao wangependa kushiriki kwenye mkutano huu watume majina yao na majimbo wanayotoka kwa namba  0653619906/0717047574. Ili kutoa muda wa kutengeneza vitambulisho vya washiriki, siku ya mwisho ya kupokea majina ya washiriki ni tarehe 01 Septemba 2016.

4.    Ikumbukwe kuwa mbali na kujadili masuala mbalimbali ya nchi na bara la Afrika, Mkutano wa Kidemokrasia ndiyo fursa pekee ya kikatiba ambapo mwanachama/mwananchi wa kawaida anayeshiriki anapata fursa ya kuwahoji ana kwa ana viongozi  wa kitaifa wa ACT Wazalendo juu ya masuala mbalimbali ya Chama.

Ado Shaibu
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma
Imetolewa leo tarehe 21 Septemba 2016.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.