ALIYEIMBA WIMBO WA DIKTETA UCHWARA MBARONI

1
Mwanamuziki wa Bongo Fleva Fulgency Mapunda maarufu Mwana Cotide amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kwa tuhuma za kuimba na kusambaza wimbo wenye maudhui ya kichochezi.
Mwana Cotide ameiamba wimbo wenye jina “Dikteta Uchwara” ambao aliusambaza kupitia mtandao wa YouTube kitu ambacho kinavunja sheria ya makosa ya mitandao.
Akisoma mashtaka hayo, mwanasheria Derrick Mukabatunzi alisema kuwa Mwana Cotide na mtayarishaji wa muziki huo, Mussa Kibakwe walitenda kosa hilo mwezi Agosti 2016 eneo la Manzese Dar es Salaam.
Watuhumiwa wote wawili walikataa mashtaka hayo na kuachiwa kwa dhamana. Kesi hiyo imetajwa kusikilizwa tena Oktoba 12.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.