CELINA PATEL BINTI WA MIAKA 11, AIBUKA KIDEDEA MASHINDANO YA KIMATAIFA YA AFRICA LIGHTING GOLDEN GOLF TOURNAMENT MKOANI ARUSHA.


Mtanzania Celina Patel binti wa miaka saba ameibuka kidedea katika mashindano ya Africa Lighting Golden Jubilee Golf Tournament yaliyofanyika mkoani arusha.

Mashindano hayo ambayo yaliwakutanisha washiriki kutoka kutoka nchi mbalimbali duniani pamoja na nchi wanachama wa jumuhiya ya afrika mashariki  ambapo mtanzania Celina Patel aliibika kuwa mshindi wa kwanza.

Kufatia Ushindi huo  Celina Patel ambye kwa kipindi kifupi ameweza kushinda medani nyingi umeleta heshima kubwa  kwa watanzania na Taifa kwa ujumla hasa katika mchezo wa golf. 

Pia Ushindi huo utakuwa chachu katika kulitangaza taifa hususani  kwa wapenzi wa mchezo huo dunia, jambo ambalo litasaidia pia kuitangaza nchi katika medani ya kimataifa hasa kupitia michezo. 

Aidha Celina Patel Ameibuka mshindi katika category mbalimbali kama Ladie Winner at Africa Lighting Golden Jubilee Golf Tournament Arusha, Junior Prize winner at Muthaiga junior Open Golf Tournament Kenya pamoja na Winner of Bronze Division at Mombasa Ladies open Golf Tournament.

Pia ni mshindi katika category ya  Junior Winner at Tanzania Open at kili golf, Winner of Women’s category in kilimanjaro Spurs Golf Tournament.
Tangu Mheshimiwa Rais ameingia madarakani,  watanzania wengi wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi

Kufatia ushindi huo ni wazi kuwa Tanzania imechukua ubingwa huo wa dunia hivyo pongezi kwa jitihada zake na kuliletea taifa ushindi huo , pia kumtakia kila la kheri katika michezo na taaluma kwa ujumla, pamoja na kukutakia Afya njema ili uzidi kuwakilisha Taifa.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.