Kaimu Meneja Kitengo cha Mahusiano kwa Umma wa BoT, Victoria Msima, akimkaribisha Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu (wa pili kushoto), kuzungumza na wanahabari kuhusu ukuaji wa pato la taifa kwa robo na nusu mwaka 2015 Dar es Salaam leo.
Taswira ya meza kuu katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Kaimu Meneja Kitengo cha Mahusiano kwa Umma, Victoria Msima,Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mabenki, Kenedy Nyoni, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Beno Ndulu na Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti wa Sera za Kiuchumi, David Kwimbere.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandshi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa ya ukuaji wa pato la taifa kwa robo na nusu ya mwaka 2016. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mabenki, Kenedy Nyoni.
Wapiga picha wakiwa kazini.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mwanahabari Samuel kutoka kituo cha Televisheni ya ESTV akiuza swali
Na Dotto Mwaibale
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesema ukuaji wa pato la Taifa umeongezeka kwa asilimia 7.9 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 5.8 kwa kipindi kama hicho mwaka 2015.
Hayo yamebainishwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu Dar es Salaam leo asubuhi wakati akizungumza na wanahabari kuhusu ukuaji wa pato la Taifa kwa robo na nusu mwaka 2016.
Profesa Ndulu alisema shughuli za kiuchumi zilizokua kwa kasi ya juu zaidi katika kipindi hicho ni usafirishaji na uhifadhi wa mizigo ikiwa ni asilimia 30.6, uchimbaji wa madini kwa asilimia 20.5, mawasiliano na habari asilimia 12.6 na sekta ya fedha na bima kwa asilimia 12.5.
Alisema ukuaji wa sekta ya uchukuzi na uhifadhi wa mizigo umetokana na kuongezekea kwa usafirishaji wa abiria kwa njia ya barabara na gesi asilia ambao umekua kwa zaidi ya nusu ukilinganisha na robo ya pili ya mwaka 2015 kwa asilimia 9.4.
"Kwa upande mwingine, ukuaji wa sekta ya uchimbaji wa madini na gesi umechangiwa zaidi na kuongezeka kwa uzalishaji wa gesi ambao umekua kutoka mmSFt3.7,793 kwa mwaka 2015 mpaka mmSFt3 11,267 kwa mwaka 2016" alisema Ndulu
Profesa Ndulu alitaja sekta nyingine ambayo imefanya vizuri ililinganishwa na kipindi kama hicho kwa mwaka 2015 kuwa ni sekta ya kilimo ambayo imekua kwa asilimia 3.2 kwa robo ya pili ya mwaka 2016 wakati mwaka jana ilishuka kwa asilimia 1.9.
Aidha sekta ya fedha na bima imekua kwa asilimia 12.5 kwa robo ya pili ya mwaka 2016 ikilinganishwa na asilimia 10.0 kwa robo ya pili ya mwaka 2015.
Akizungumzia ukuaji wa pato la Taifa alisema katika nusu ya mwaka 2016 yaani Januari hadi Juni 2o16 kasi ya ukuaji wa pato la taifa imeongezeka na kufikia asilimia 6.7 ikilinganishwa na asilimia 5.7 kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment