Hali ilivyokuwa katika makao makuu ya chama cha wananchi Cuf majira ya asubuhi ya saa mbili leo ambapo Mwenyekiti wa chama hicho anayedaiwa kutimuliwa uawanachama akiwasili ofisini kwake baada ya kuwepo Taarifa za ugeni kutoka zanzibar ukiongozwa na Katibu mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad ambapo alitarajiwa kuwasili katika ofisi hizo baada ya kutoka katika kikao cha baraza kuu walioamua kumtuimua Lipumba juzi.
Akizngumza na wanahabari mapema asubuhi hiyo amewaeleza wanahabari kuwa Hana Taarifa zozote za kuwa na ugeni huo lakini Ndani ya makao makuu hayo kuna Ofisi za katibu mkuu wa chama hivyo haonijambo la ajabu kama anakuja ofisini kwake na anamsubiri kwa hamu ili ampe mikakati na mipango ya chama inavyokwenda kwa ajili yab kukuza chama chao.
Ameasema kuwa yeye na maalim Seif hawana ugomvi kama inavyoelezwa katika vyombo vya Habari bali kinachowachanganya watu ni yeye kufwata katiba ya chama ambayo imemtruhusu kurudi madarakani baada ya kujiulzuli mwaka jana.
Amesema kuwa anashangwazwa kusikia kuwa Ktibu mkuu wake anaenda kuomba Ulinzi kwa polisi kwa ajili ya kuja ofisini kwake wakati yeye ana walinzi wa serikali,ana walinzi wa chama na hakina mtu anayeweza kuleta fujo kwa kuwa chama hipo chini ya ulinzi mkali wa walinzi wa chama hicho
Hadi tunaondoka eneo la tukio Maalim Seif hakuwa amefika katika ofisi hizo na hali ilikuwa swari
No comments:
Post a Comment