Monday, September 26, 2016

Picha-Sherehe za miaka 21 ya LHRC,waitumia kuwasaidia watoto wa Makao ya Taifa ya watoto kurasini

Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha sheria na haki za Binadamu nchini Tanzania LHRC akimkabidhi zawadi mbalimbali Beatrice Laurence ambaye ni Afisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya watoto Kurasini Jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 21 tangu kuanzishwa kwa LHRC ambapo sherehe hizo wameamua kuzifanya kwa staili ya kuwasaidia watoto hao waliopo katika kituo hicho cha serikali na kufurahi nao pamoja leo
Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania LHRC akimkabidhi zawadi  mmoja wa watoto ambao wanalelewa katika Kituo hicho cha watoto kilichopo Kurasini Jjini Dar es salaam leo ikiwa LHRC wanatimiza miaka 21 ya kuzaliwa kwao
Baadhi ya Vifaa mbalimbali vilivyotolewa na LHRC kwa watoto hao wanaoishi katika makao ya Taifa ya watoto Kurasini Jijini Dar es salaam vikiwemo vyakula,vifaa vya usafi na mahitaji mengine kwa watoto hao ikiwa ni ishara ya upendo na kuwakumbuka watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini pamoja na ishara ya kusherehekea miaka 21 ya kuanzishwa kwa LHRC nchini Tanzania

Watoto wanaoishi makao ya taifa ya watoto Kurasini Jijini Dar es salaam wakisikiliza kwa makini wakati viongozi wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC walipokuwa wanazungumza nao walipowatembelea kituoni kwao kusherehekea nao kuadhimisha miaka 21 ya LHRC ambapo watoto hao wamepata fursa ya kuzungumza na maafisa hao na kupokea zawadi mbalimbali kutoka kwao ikiwa ni ishara ya upendo kwa watoto hao




Muda wa Keki 

No comments: