Chama cha democrasia na maendeleo chaema hatimaye leo kimatangaza kufuta rasmi maandamano na mikutano ya hadhara iliyokuwa imepewa jina la UKUTA na abadala yake wameamua kutumia mbinu nyingine walizozitaja kuwa bira zaidi za kufikisha ujumbe waliokusudia kufikisha kwa serikali.
Akizngumza na wanahabari mapema leo Mwenyekiti wa chama Taifa Mh Freman Mbowe amesema kuwa Baada ya kuspgeza mbele maandamano hayo na kuwapa nafasi viongozi wa Dini kulifanyia kazi swala hilo hatimaye wamegundua kuwa hakuna chochote kilichofanyika ambapo ni haki yao kuendeleaza Fikra za UKUTA kwa kuwa wametumia kila mbinu kulimaliza lakini imeshindikana.
Amesema kuwa Swala la kudai Haki za msingi sio swala la siku moja hivyo Fikra za kudai haki na operation UKUTA zinendelea kudumu na kutumia mbinu nyingine mpya kwa ajili ya kudai haki ya kidemocrasia ambayo imeminywa nchini.
Akieleza mbinu hizo mpya amesema kuwa chama sasa kimeanza ziara za kwenda katika mataifa ya ulaya na jumuiya za ulaya kuwaeleza nkile abacho kinaendelea nchini Tanzania na kufanya ikutano mbalimbali kuonyesha hali halisi ambapo kwa kuanza na hili kundi la kwanza la viongozi wakuu wametoka Ujerumani kufanya hivyo na ziara Hizo zitakuwa nyingi Zaidi.
Njia nyingine amesema kuwa wameamua kufungua kesi mbalimbali na nyingi katika mahakama za ndani na nje kwa ajili ya bkupinga yale abayo hayaendi sawa katika taifa kwa sasa ikiwemo kuminywa kwa Democrasia ya nchi.
NUKUU
Kuhusu ukuta tulikubaliana kuwapa muda viongozi wa dini kufanyia kazi hilo.
Jana tulikutana tena kupata mrejesho wa swala hilo.
Taarifa ambazo kamati maalum ya kamati kuu imepewa taarifa kuwa vingozi wa dini hawakufanya lolote hatuna taarifa.
Sisi kama chama cha siasa tuliwsheshimu na tutaendelea kuwaheshimu sana ila ni wajibu wetu sasa kuendelea na haraksti zetu
Baada ya kuona mambo kadhaa yalitopo tumeona kusitisha maandamano ya October moja na kupisha mbinu nyingine mpya
Tukio la kudai haki sio tukio la Siku moja kama wengi wanavyodhani.
Kwa umuhimu wa hali hiyo chama kilituma Ujumbe maalum Ulaya kuielezea Jamii ya kimataifa ugandamizaji unaoendelea nchini.
Bado misafara mingine ya chama itaendelea kwenda nchi nyingi zaidi kufanya mikutano na kuzitaka jumuiya nzima za kimaraifa waelewa kuwa tanzania ile Amani haipo tena
Tunaendelea na maandalizi ya kufungua kesi mbalimbali kuhusu yanayoendelea nchini.
TAKE NOTE....UKUTA WA OCTOBER MOJA UMEFUTWA RASMI WAMETANGAZA KUFANYA MBINU NYINGINE.
Kuhusu sakata la Lipumba na Cuf Mbowe anasema ----.....Lipumba ni political relevant amepoteza kisiasa.ni wakala wa wasaliti wenzake.tunampuuza maana kuendelea kumjadili ni kumpa nafasi ambayo alikuwa nayo zamani.sisi tutaendelea kushirikiana na Cuf na kuheshimu vikao vyake halali.
Kuhusu Report ya Twaweza anasema kuwa nao wamejitwishwa uwendawazimu.ni mtanzania mwendawazimu pekee anayeweza kuiamini report yao.eti serikali inakubalika kwa asilimia 95 ni uwendawazimu Mkubwa sana.Twaweza wanaandaliwa report na serikali.wanalipwa na serikali.hawawezi kuja na fact
No comments:
Post a Comment