Ndege mpya ya serikali, Bombardier Q400 ikiwa katika uwanja wa Dar es Salaam mchana huu
Ndege ya kwanza kati ya mbili zilizoagizwa na serikali, aina ya Bombadier Q400 kutoka nchini Canada tayari imewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam.
Ndege hizi mbili zimenunuliwa kulifufua shirika la ndege la Tanzania (ATCL) ambalo kwa sasa lina ndege mbili, ambayo moja ni ya kukodi. Ujio wa ndege hizi mbili umeelezwa kuwa umelenga kusaidia katika soko la ndani, na kusaidia kurahisisha usafiri wa anga kwenda maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Ndege hizi zitakuwa na uwezo wa kutua katika viwanja vingi nchini kwani huhitaji takribani barabara ya urefu wa kilomita 1 tu kuweza kuruka tofauti na ndege zinazotumia jet engine ambazo huhitaji zaidi ya barabara yenye urefu wa kilomita 2 kuweza kuruka.
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akisalimiana na Rubani aliyerusha Ndege mpya moja kati ya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016. |
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine wakiwa kwenye Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo Septemba 20, 2016 |
No comments:
Post a Comment