Tuesday, September 20, 2016

WANACHOKIFANYA VIONGOZI WA CHADEMA NCHINI UJERUMANI


Viongozi wa JUU wa CDM wakiongozwa na katibu mkuu Dr. Vicent Mashinji wapo nchini Ujerumani leo tarehe 18/09/2016,kuitikia mwaliko wa bunge la Nchi hiyo lililotaka kujua kile walichokuwa wanakisikia kama mkwamo katika siasa za kidemokrasia nchini.
Viongozi hao ni pamoja na John Mrema (Mkuu wa Idara ya habari,protokali na Mambo ya nje),Benson Singo Kigaila(Mkurugenzi wa ulinzi na Usalama),John John Mnyika (Naibu katibu Mkuu),Tundu Antipas Lisu(Mnadhimu na Mwanasheria wa CDM),Pro.Baregu(Mjumbe wa kamati kuu) Bi Zauda( Makamu bavicha Zanzibar)
Wengine ni Wabunge,
Mh.Anatropia Theonest, Mh.Cecilia Pareso na Mh Ruth Mollel.
Ziara hii ya viongozi wa CDM inatarajiwa kukutana na makundi mbalimbali katika Nchi ya Ujerumani kama ratiba inavyoonekana.
Wanatarajia kukutana na Bunge la nchi hiyo,wizara mbalimbali, delegation ya EU,taasisi za serikali n kibinafsi sambamba na vyombo vya habari.
Leo ni siku ya pili ya ziara ya viongozi wa CDM(19/09/2016) na Wenyeji wetu(Germany),tumefanya yafuatatayo:
1)Mazungumzo kati ya delegation ya Tanzania na waandishi wa habari wa hapa(Germany)
2) Mawasilisho na discussion na Mawaziri mbalimbali.
3)Discusion na makundi mbalimbali juu ya hatma ya Demokrasia ya Tanzania.
Ikumbukwe,hii ni ziara rasmi ya viongozi wa ngazi ya juu wa CDM na wabunge pamoja na serikali ya Shirikisho ya Nchi ya UJERUMANI.

No comments: