MAPOKEZI MAKUBWA KUWAPOKEA WALIOMTIMUA LIPUMBA JANA YAJA


Wanachama wa CUF wa mkoa wa Dar Es Salaam kwa kushirikiana na Wabunge wote wa CUF, wameandaa mapokezi makubwa siku ya Ijumaa (Tarehe 30 Sept) saa 2.00 asubuhi ambapo watawakaribisha Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa katika Ofisi Kuu za CUF Buguruni, Wajumbe wa Baraza watakuwa wanatoka Zanzibar kwenye Kikao Maalum kilichotengeneza Mustakabali muhimu wa chama.

Mameya wa CUF, Madiwani, Kamati ya Uongozi ya Chama, Katibu Mkuu, Wakurugenzi, Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Chama na watu muhimu watafika Buguruni Ofisini na kuanza kazi. Mjulishe kila mwana CUF ahudhurie.
Imetolewa na Wanachama na Wabunge wa CUF.
27 Sept 2016.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.