Wednesday, September 28, 2016

Ababu Namwamba Ndani ya Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia Nchini.



"Tanzania ikichangaruka (ikichangamka), Uganda, Kenya na Nyasa (Malawi) zitaumana (zitashikama kuamka kudai Uhuru na Maslahi ya Wanyonge)" - aliimba Mwanamuziki wetu Frank Joseph Humplick mashuhuri Kwa jina "Chotara wa Kichaga"

Afrika Mashariki inaamka, Siasa za Uwajibikaji na Kulinda Maslahi ya Wanyonge wa Afrika Mashariki zinaanza kushika hatamu. Jahazi likibebwa na Vijana wa Mataifa ya Afrika Mashariki.


Nchini Kenya Ndugu yetu Pius Tawfiq Ababu Namwamba anaongoza Jahazi la Vijana wa Nchi hiyo wanaodai Mabadiliko ya Kiuwajibikaji na Siasa za Maslahi ya Umma wa Kenya na Afrika Mashariki kwa Ujumla. Ababu Mwenye Miaka 40 na ambaye ni Kiongozi wa Chama Cha Wafanyakazi Cha Kenya (Kenya Labour Party) amepitia mengi mno:

• Amekuwa Mbunge wa Jimbo la Budalang'i Kupitia Chama cha ODM tangu Mwaka 2007 mpaka sasa.
• Amekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Kenya Juu ya Maandalizi ya Katiba Mpya ya Nchi hiyo.
• Amekuwa Waziri wa Michezo na Vijana Katika Serikali ya Mseto ya Rais Mwai Kibaki.

• Amekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu Za Mashirika ya Umma ya Kenya (PAC).
• Amekuwa Katibu wa Umoja wa Kamati za Hesabu za Mashirika ya Umma za Mabunge ya Afrika Mashariki (EAPAC).
• Amekuwa Katibu wa Kamati ya Wabunge wa Chama Cha ODM.
• Na Sasa ni Kiongozi wa Chama Cha Wafanyakazi Cha Kenya (Kenya Labour Party).

Stori ya Maisha na Uzoefu wa Ababu ambaye ni Mwanasheria Kitaaluma ina mafunzo mengi Kwa Vijana wa Tanzania, ikionyesha Uvumilivu, Weledi, Ustadi, Kuanguka na Kusimama, pamoja na Uzalendo kwa Taifa lake - akisimama dhidi ya yoyote na lolote lisilo na Maslahi kwa Umma. Ni mafunzo ambayo yana faida kwa Kizazi Kipya Cha Afrika Mashariki.

Chama Chetu cha ACT Wazalendo, kimeamua kuwa Daraja la Kuyaleta Mafunzo ya Maisha ya Ababu Kwa Wananchi wa Tanzania na Afrika Mashariki Kwa Ujumla kwa kumleta Ababu Katika Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia.
Lini: Oktoba 8, 2016.
Wapi: Jijini Dar es salaam.
Kushiriki: Jiandikishe kushiriki kwa namba 0653619906 (Katibu Mwenezi Taifa) au 0717047574 (Katibu wa Vijana).
Karibuni Sana

No comments: