Saturday, September 17, 2016

MREMBO TOKA IRINGA AIBUKA KIDEDEA MSHINDI WA TTCL MISS HIGHER LEARNING 2016

 MLIMBWENDE Laura Kwai kutoka Chuo Kikuu cha Iringa amefanikia kunyakua taji la TTCL Miss Higher Learning 2016 akiwabwaga washiriki wenzake Evelyn Andrew aliyeshika nafasi ya pili na  Clara Nyaki aliyekuwa watatu.
Mashindano hayo yaliyofanyika Jana usiku katika Ukumbi wa King Solomon yaliweza kufana hasa baada ya kuwa na ushindani wa hali ya juu baina ya warembo hao.
Katika meza ya Majaji iliyoongozwa na Hasheem Lundenga iliweza kufanya kazi kubwa kwa kuweza kuwataja washiriki walioingia tano bora na hatimaye mshindi wa TTCL Miss Higher Learning 2016 kuwataja Washiriki waliofanikiwa kuingia ni tano bora ambao Mariam, Lucy Ludy, Evelyn Andrew, Laura Kwai na Clara Nyaki .

Mshindi wa kwanza amejinyakulia kiasi cha shilingi Milioni Moja taslimu (1,000,000) pamoja Scholarship ya kusoma katika Chuo chochote, mshindi wa pili amejinyakulia milioni moja taslimu (1,000,000)na mshindi wa tatu amepata Laki saba (700,000) taslimu na kwa Washiriki waliobaki kila mmoja atakabidhiwa kiasi cha laki mbili kila mmoja (200,000).
Tanzanite International Film Festival (TAIFF) walimtaja Laura Kwai na Rhoda Iddy Kama mabalozi wao katika kuyatangaza madini ya Tanzanite ndani na nje huku TTCL wakimtaja Glory Gideon kama balozi wao kwa muda wa mwaka mmoja.

Walimbwende walioshiriki kinyang'anyiro cha Kumsaka TTCL Miss Higher Learning 2016 ni Glory Gideon (Chuo cha Usimamizi wa fedha IFM), Lucy Ludy (Taasisi ya Ustawi wa Jamii), Jonatha Joram (Chuo cha Usimamizi wa fedha IFM), Clara Nyaki (Taasisi ya Ustawi wa Jamii), Rhoda Iddy (CBE), Evelyne Andrew (Taasisi ya Ustawi wa Jamii), Tamita Mwakitalu (Chuo cha Utumishi wa Umma, Magogoni), Jackline Everist (Chuo cha Usimamizi wa fedha IFM), Nasra Muna (Chuo cha Usimamizi wa fedha IFM) Laura Kwai (Iringa University), Mariam J Mwita (Chuo cha utumishi wa Umma, Magogoni), Emmaculate Kasinsa (Chuo cha utumishi wa Umma, Magogoni), Victoria Shiyo (CBE), Farida mlawa (UDOM), Lilian  Kaishozi (UDOM).


No comments: