Thursday, September 15, 2016

Taarifa Nyingine Kuhusu Malori Yaliyotekwa Congo na Madereva wao

Hii ni Taarifa Fupi kutoka kwa Kutoka chama cha wamiliki wa Malori Tanzania.
  
Tumezungumza na mmiliki wa kampuni ya Simba Logistics Mzee Azim Dewji amethibitisha taarifa hizi na tayari tumezungumza na balozi wa Tanzania DRC pamoja na wizara ya mambo ya nje tayari serikali inashughulikia swala hili. Jumla ya gari zilizotekwa ni 12 kati ya hizo gari 8 za Tanzania na 4 za Kenya. 

Gari 4 za Tanzania zimechomwa moto na madereva wote walichukuliwa na waasi lakini bahati nzuri madereva wawili wa Tanzania walifanikiwa kuwatoroka. Tukio limetokea sehemu inaitwa Kasebebena na Matete kilometer 30 kutoka mji wa Namoya. 

Tunawashauri wanachama waliopakia mzigo kuelekea huko kuwasiliana na madereva wao wasitishe safari ili kusubiri taarifa ya hali ya usalama kutolewa.

No comments: