SERIKALI imesema imepokea taarifa za kutekwa kwa malori 12 katika
eneo la Namoyo lililopo Jimbo la Kivu ya Kusini nchini Kongo DRC jana na
jitihada za kuwaokoa madereva hao zinafanywa kupitia nchi zote mbili.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiriakiano wa
Afrika Mashariki, Mindi Kasiga amesema malori hayo yanamilikiwa na
mfanyabiashara Azim Dewji na mfanyabiasha wa Kenya.
Mindi amesema taarifa zilizopatikana zinasema watekaji ni kikundi cha
waasi cha MaiMai ambapo baada ya kuyateka magari hayo waliwashusha
madereva na kuwapeleka porini na kisha kuyateketeza kwa moto malori
manne ambayo yanamilikiwa na Dewji.
“Waasi hao wametoa saa 24 kuanzia jana saa 10 jioni walipwe fedha
kiasi cha dola za kimarekani 400 sawa na Sh milioni 8.7 kwa kila dereva
ili waweze kuwaachia,”amesema Mindi.
Amesema serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki imechukua hatua za awali za kuwasiliana na serikali ya
Kongo DRC.
USIKOSE KUSUBSCRIBE YOUTUBE ACOUNT YETU HABARI24 TV
USIKOSE KUSUBSCRIBE YOUTUBE ACOUNT YETU HABARI24 TV
No comments:
Post a Comment