.

Tizama Maswali aliyoulizwa Lipumba Leo Redioni Jinsi alivyoyajibu
SWALI: Je, una uthibitisho kwamba Lowassa ana makosa na anapaswa kupelekwa mahakamani?

JIBU: Hilo mimi sijui, hilo ni la mahakama


SWALI: Sasa Kwanini unasema hafai?

JIBU: Hiyo Mwalimu Nyerere ndiye aliyesema kwamba huyu ana kipato kikubwa ambacho haijulikani amekipataje, sasa kama hadi mwalimu Nyerere alikuwa hamkubali, mimi nitamkubali vipi
SWALI: Kama utarudi CUF, halafu Lowassa akateuliwa na CHADEMA kugombea urais, utamuunga mkono?

JIBU: Kwenye uchaguzi wa 2020 sina mpango wa kumpisha Lowassa kwenye chama cha CUF na wala siwezi kumuunga mkono.
SWALI: Lakini CUF si itakuwa kwenye UKAWA
JIBU: UKAWA ilikuwa kwenye Bunge la Katiba kusimamia maadaili.
SWALI: Kwani ndani ya CUF hakuna mtu mwingine yeyote anayeweza kuwa mwenyekiti?
JIBU: Siyo kwamba mimi napenda sana kugombea, Niliwahi kumwendea Warioba kwamba anaweza kugombea, lakini pia nilishamwendea Dkt. Salim Ahmed Salim baada ya kukatwa CCM, nilimuomba aje agombee CUF ili kuimarisha muungano, akasema hawezi kwa kuwa yuko CCM.
SWALI: Nini hatma yako kisiasa?
JIBU: Hatma yangu iko kwa Msajili wa Vyama vya Siasa
SWALI: Je unaweza kuanzisha chama kingine au kuhamia chama kingine?
JIBU: Sina mpango wa kuanzisha chama kingine chocho, wala sina mpango wa kuhamia chama kingine chochote.
SWALI: Uko tayari kumaliza bifu na Maalim Seif
JIBU: Ilikuwa ni makosa sana kwa maalim kukataa kumpa mkono Dkt Shein, huwezi kupeleka tofauti za kisiasa msibani.
SWALI : Jumuiya ya Wanawake CUF inasema haikuungi mkono...
JIBU: Jumuiya gani hiyo ya wanawake ambayo inamtenga na inataka kumfukuza Magdalena Sakaya, Sakaya ndiye jembe katika wabunge wote wa CUF. Maftah wa mtwara, kijana shupavu ambaye alizhinda ubunge licha ya kuwekewa wagombea wengine wa UKAWA, CHADEMA waliweka mgombea ili kumuangusha Maftah, sasa ukiwafukuza hao utabaki na nini. Wanataka CUF Bara ife, yaani wanaiuza CUF kwa bei poa kwa CHADEMA na Lowassa

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.