Monday, September 19, 2016

WAJUMBE WA BODI YA RUFANI ZA KODI WAPATIWA MAFUNZO

manamboHivi karibuni kumetokea mabadiliko kadhaa katika sheria za kodi ikiwa ni pamoja na kodi ya ongezeko la thamani hali inayopelekea Chuo cha Kodi kutoa mafunzo kwa taasisi za serikali ili kuzitambua sheria hizo kinagaubaga.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu kutoka Wizara wa Fedha Gidion Manambo amesema kuwa kuzifahamu kwa ufasaha sheria za kodi ni kipengele muhimu katika kutoa maamuzi baada ya kusikiliza mashauri ya kodi, hivyo basi uamuzi wa maafisa hao kurudi chuoni kuzipitia tena sheria za kodi ni mfano wa kuigwa.

Aidha Manambo ameongeza kuwa mafunzo hayo yataongeza tija na ufasaha katika kutekeleza majukumu ya watendaji hao kwa kurahisisha maamuzi ya rufaa ili serikali ipate mapato yake kwa wakati.

“Ili kuweka mezani sawa kati ya serikali ambayo ndiyo inakusanya kodi kutoka kwa mlipakodi ambaye ni mfanyabiashara ndiyo maana ilianzisha chombo hiki ili kuhakikisha kwamba mlipakodi analipa kodi stahiki na serikali inapata mapato yake kwa mujibu wa sheria za kodi”alisema Manambo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo amesema Chuo hicho kinaona fahari kutoa mafunzo hayo kwa taasisi za kiserikali kama Bodi ya Rufani za kodi kwani mafunzo hayo ni njia mojawapo ya kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi.

No comments: