Sunday, October 2, 2016

MEYA WA DAR ES SALAAM AWATAKA WAZAZI KUTUMIA MUDA MWINGI KUWAFUNDISHA WATOTO WAO MAADILI MEMA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgi9ArcHIt97iCAxsFNNvnnTCk5QdVi2khUo6zFHwEc9LwnCzIT3CC6oL_SYRYTenyYYNsWVBUURthObyh9ngs_NMSGPtMMket2RuUSuwY5vihYZ-KF-LuTYf6jg1u76WeFpLTfq52Ax30/s1600/1.jpg
NA MWANDISHI WETU,Dar

WAZAZI wametakiwa kutumia muda mwingi kuwafunisha watoto wao maadili mema ili

kuepuka kuwa na Taifa lenye watumishi ambao hawana maadili.

kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita

wakati wa mahafali ya wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Amka

iliyopo Kigamboni jijini hapa.

Isaya alisema watoto wanapomaliza shule huwa na tabia nje kutokana na maadili

ambayo anafundishwa na walimu wao wakiwa shuleni lakini wazazi wanashindwa

kuendeleza nizamu zao na hivyo kujikuta wakijiingiza kwenye makundi yasiyokuwa na

maadili.

Alisema wanafunzi ambao wanamaliza elimu ya msingi ndio wanategemewa na Taifa kuwa

viongozi wa badae na kwamba kama wazazi wasipotunza nidhamu za watoto taifa

linaweza kukosa viongozi ambao hawana maadili.

" Wazazi tusaidiane, kutunza nidhamu ya watoto wetu, walimu wanajitahidi

kuwafundisha maadili mema,na hawa ndio viongozi wetu,hakuna wengine kama

tutashindwa kutunza hiki ambacho wamekipata kutoka kwa walimu ni dhahiri kwamba

tutakosa viongozi wenye maadii na Taifa kulipeleka sehemu mbaya" alisema Isaya.

Akizungumzia shule ,Isaya alisema imefika wakati sasa kila mzazi aone umuhimu wa

kujenga shule za kata kutokana na kwamba bado serikali inajukumu kubwa la

kuhakikisha kwamba shule hizo zinakuwa bora kama ilivyo kwa shule ambazo zinamilika

na watu binafsi.

Alisema anafahamu kwamba wapo watu ambao wanauwezo wa kuisaidia serikali badala ya

kusubiri kila kitu kifanyike kupitia serikali na kwamba kwakuisaidia itakuwa ni

njia moja ya kujenga Taifa ambalo linajali maendeleo ya wananchi.

" Tuwe na utamaduni, leo hii ukipita nakuona kwamba kuna shule ambayo haina

madarasa ya kutosha, ukanunua mabati kadhaa ukapeleka utakuwa umesaidia watoto

ambao wanasoma pale badala ya kusubiri serikali ije kufanya, nayo ina mambo mengi"

aliongeza.

Hata hivyo Meya Isaya aliahidi kuchangia shule hiyo Kompyuta tano hatua ambayo

ilitokana na risala iliyosomwa ambayo ilieleza kuwepo ka mkakati wa kujenga chumba

cha kompyuta kwa ajli ya kufundishia wanafunzi.

sambamba na hilo, alisema kwamba anafahamu mchango unaotolewa na shule binafsi na

kwamba hiyo ni changamoto pia kwa shule za serikali kufanya vizuri kwenye mitihani

yao kama ambavyo inatokea kwenye shule hizo.

Awali akimkaribisha Meya wa Jiji , Meneja wa shule hiyo Dk. John Makoa pamoja na

mambo mengine  alimpongeza kwa kuchaguliwa kuwa meya wa jiji na kusema kwamba

anatambua juhudi zake za kufanya kazi na kwamba wananchi wa Dar es Salaam

wanatakiwa kujivunia kupata kiongozi kama yeye.

mwishoo.

No comments: