Sunday, November 6, 2016

HABARI MCHANGANYIKO KUTOKA TFF


MSUVA MCHEZAJI BORA WA VPL MWEZI OKOTOBA


Winga Simon Msuva wa Young Africans amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Msuva alikuwa na washindani wa karibu wawili katika kinyang'anyiro hicho cha Oktoba ambao wote ni kutoka Simba. Wachezaji hao ni Shiza Kichuya na Mzamiru Yassin.

Katika mwezi Oktoba ambao ulikuwa na raundi sita, Msuva aliisaidia timu yake kupata jumla ya pointi 14 huku akifunga mabao manne, na kutoa pasi tano za mwisho (assist).

Kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi, Msuva ambaye alikuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2014/2015 atazawadiwa kitita cha sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.



MCHEZO KATI YA BULYANHULU, GREEN WARRIORS

Mchezo Na. 4 wa Ligi Daraja la Pili kati ya Bulyanhulu na Green Warriors ulikuwa ufanyika jana Novemba 4, 2016 kwenye Uwanja wa CCM-Kambarage, mkoani Shinyanga haikufanyika.

Mchezo huo haikufanyika kwa sababu ya kukosa mawasiliano kati ya msimamzi wa kituo huko Shinyanga, Kamisaa na Mchezo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kwa taarifa hii, TFF inapenda kufahamisha familia ya mpira wa miguu kuwa mchezo huo utafanyika hapo baadaye kwa kupangiwa tarehe nyingine mpya baada ya kuondolewa kwa changamoto inayohusu leseni za wachezaji ambazo ziko tayari shirikishoni.


ELIGIBILITY OF CONGO U17 PLAYERS

Following various reports circulating in the social media regarding the eligibility of Republic of Congo U17 players in the just ended Afcon U17 qualifiers Tanzania Football Federation wishes to state as follows:

Eligibility player (s) is a matter of control under the Confederation of African Football CAF.

TFF is in contact with CAF regarding the subject matter referred above. TFF wishes to reiterate its willingness to continue to cooperate with CAF in its endeavors to ensure CAF and FIFA tournaments are organized in a fair manner.

Consequently all matters related to eligibility of players in various CAF organized tournaments should be referred to CAF offices.

AZAM SPORTS FEDERATION CUP KUZINDULIWA TANGA NOVEMBA 19, 2016

Azam Sports Federation Cup (ASFC) itakayoshirikisha timu 86 msimu huu, itaanza rasmi Novemba 19, 2016 kwa uzinduzi rasmi utakaofanyika mkoani Tanga.

Bingwa wa Mkoa wa Tanga msimu 2015/2016, Muheza United itacheza Sifa Politan ambayo ni Bingwa wa Temeke, Dar es Salaam – mchezo utakaofanyika Uwanja wa Mkwakwani jijini humo.

Siku hiyo kabla ya mchezo kutakuwa na shamrashamra kupamba michuano hiyo  zitakazoandaliwa na Wadhamini Azam Tv ambayo kwa msimu wa 2016/17 zimeongezwa timu 22 kutoka mabingwa wa mikoa-- Muheza na Sifa Politan ni miongoni mwa timu hizo. Ongezeko hilo tofauti na msimu uliopita ambako kulikuwa na timu 64.

Mwaka huu kuna timu 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL); timu zote 24 za Ligi Daraja la Kwanza (FDL), timu zote 24 za Daraja la Pili (SDL) na timu 22 za mabingwa wa mikoa. Mashindano hayo yatakuwa ni ya mtoani na yataendeshwa kwa raundi tisa (9).

Raundi ya Kwanza itashirikisha timu zote 22 za Mabingwa wa Mikoa katika makundi manne ya timu sita na timu tano ambako timu mbili za juu zitaingia raundi ya pili.

Raundi ya Pili itashirikisha timu nane zilizofuzu za RCL katika raundi ya kwanza na kujumlisha timu 24 za Daraja la Pili (SDL) kufanya jumla ya timu zote kuwa 32 kwa hatua ya pili.

Raundi ya Tatu itashirikisha timu 16 zilizofuzu hatua ya pili kushindana ili kupata timu nane zitakazoingia hatua ya nne.

Raundi ya Nne itashirikisha timu zote za Daraja la Kwanza (24) na kumulisha timu nane (8) zilizoshinda Raundi ya Tatu (3) kufanya timu zote kuwa 32.

Raundi ya Tano, itashirikisha timu 16 zilizofuzu Raundi ya Nne (4) na kumuisha timu zote 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kufanya timu zote katika raundi hii kuwa 32.

Raundi ya Sita itashirikisha timu zote 16 zilizofuzu katika Raundi ya Tano na mzunguko huo utaitwa Hatua ya 16 Bora.

Raundi ya Saba (7) itashirikisha timu nane zilizofuzu katika raundi ya sita na mzunguko huo kutambuliwa kuwa Nane Bora au Hatua ya Robo fainali .

Raundi ya Nane ambayo itashirikisha timu nne zilizofuzu Raundi ya Saba (Robo Fainali) na mzunguko huo utatambuliwa kuwa ni Nusu Fainali.

Raundi ya Tisa itashirikisha timu mbili zilizofuzu Raundi ya Nane na washindi hao wa Nusu Fainali na kumpata Bingwa wa Azam Sport Federation Cup kwa msimu wa 2016/2017.


LIGI YA VIJANA KUANZA KUPIGWA NOVEMBA 15, 2016

Ligi ya Vijana ya Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF) wenye umri wa chini ya miaka 20, inatarajiwa kuanza Novemba 15, 2016 mwaka huu kwa uzinduzi rasmi utakaofanyika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera kwa timu za vijana za Kagera Sugar na Young Africans ya Dar es Salaam kuchuana siku hiyo.

Timu hizo ambazo zimepangwa kundi A, zitaanza mchezo wao siku hiyo saa 10.30 jioni (16h30) ikiwa ni baada ya shamrashamra za uzinduzi wake. Kwa kuwa itakuwa ni uzinduzi, basi siku hiyo kutakuwa na mchezo mmoja tu, lakini kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Bodi ya Ligi ya TFF kwa siku kutakuwa na michezo miwili kwa tofauti ya saa – mchana na jioni.

Mbali ya Kagera Sugar na Young Africans, timu nyingine ambazo zitakuwa kwenye kundi hilo la A ni Stand United na Mwadui za Shinyanga ambazo zitacheza siku inayofuata (Novemba 16, 2017) saa 10.30 jioni na kwa kukamilisha raundi ya kwanza kwa kundi hilo, Novemba 17, mwaka huu Azam itacheza na Mbao FC katika mchezo utakaopigwa saa 8.00 mchana (14h00) kabla kuzipisha Toto Africans na African Lyon saa 10.30 jioni.

Kwa upande wa Kundi B ambalo kituo chake rasmi kitakuwa Dar es Salaam, Simba itafungua dimba na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Uhuru jijini - mchezo utakaonza saa 8.00 kabla ya kuzipisha timu za JKT Ruvu na Ruvu Shooting kucheza saa 10.30 jioni siku hiyo hiyo.

Ili kukamilisha mzunguko wa kwanza, siku inayofuata Novemba 17, mwaka huu Tanzania Prisons itacheza na Mbeya City saa 8.00 mchana (14h00) wakati Majimaji itacheza na Mtibwa saa 10.30 jioni.

Ligi hiyo ya mkondo mmoja, hatua ya makundi inatarajiwa kufikia ukomo Desemba 12, 2016 ambako timu nne vinara kutoka katika kila kundi zitapangiwa ratiba mpya na kituo ili kutafuta bingwa wa msimu kwa timu za vijana. Kituo hicho kitatangazwa baada ya kumalizika hatua ya makundi hapo Desemba 12, mwaka huu.

Ujio wa ligi hiyo ni utekelezaji au kukidhi matakwa ya maelekeo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) katika kategori ya uwepo wa timu za vijana zinazoshindana mbali ya kupata huduma za shule na matibabu kwa timu zote za Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi daraja la Kwanza.

..……………………………………………………………………………………………..
ISSUED BY TANZANIA FOOTBAL FEDERATION

No comments: