Monday, November 28, 2016

Haya ndiyo yaliyojiri kwenye soko la hisa wiki hii kuisha Ijumaa tarehe 25 Novemba 2016.

Mauzo ya Soko
Idadi ya mauzo imepungua kwa asilimia 87% na kufikia TZS 0.5 Bilioni kutoka TZS 4 Bilioni wiki iliyopita.
Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa pia imepungua kwa asilimia 85% hadi Laki Moja (101,809) kutoka Laki Sita (671,618) wiki iliyopita.

Hata hivyo kushuka kwa mauzo ya hisa kunaweza kuhusianishwa na ongezeko la mauzo ya hati fungani. 

Wiki hii hati fungani nne (4) zimeuzwa na kununuliwa kwenye soko kwa thamani ya TZS 22.1 Bilioni, ambalo ni ongezeko la asilimia 33% ya thamani ya mauzo katika soko la hati fungani kutoka mauzo ya wiki iliyopita ambapo hati fungani sita (6) ziliuzwa na kununuliwa kwa thamani ya TZS 16.6 Bilioni

Kampuni tatu zilizoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni zifwatazo:
1.     DSE kwa asilimia 37.74%
2.     TBL kwa asilimia 21.39%
3.     CRDB kwa asilimia 13.33%

Ukubwa wa Mtaji wa Soko
Ukubwa wa mtaji wa soko umeshuka kwa wastani wa asilimia 2.5% hadi Trilioni 20.4 kutoka Trilioni 20.9 wiki iliyopita.
Ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani umeendelea kubaki kwenye kiwango kile kile cha Trilioni 8.1 wiki hadi wiki.

Viashiria (Indexes)
Sekta ya viwanda imeendelea kubaki kwenye wastani ule ule wa TZS 5,031 wiki hadi wiki.

Sekta ya Huduma za Kibenki na Kifedha imeshuka pointi 0.52 kutokana na kupungua kwa bei za hisa za DSE kwa asilimia 1.59%.

Sekta ya Huduma za Kibiashara wiki hii imeendelea kubaki kwenye wastani ule ule wa TZS 3,157 sawa na wiki iliyopita.

Ingawa idadi ya mauzo ya hisa imeshuka kwa asilimia 87%, idadi ya mauzo ya hati fungani imeongezeka kwa asilimia 33%.

No comments: